Na Woinde Shizza, Arusha
Imebainika
kuwa Jukumu la kulinda na kuenzi amani ambayo ni tunu kwa taifa letu ni
la kil a wananchi na sio la serikali peke yake.
Hayo
yamebainishwa leo na mkuu wawilaya ya monduli Iddi kimanta akiongea na
wananchi Pamoja maafisa wajeshi wakati wa sherehe za maadhimisho ya
miaka 42 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho Pamoja na kilele cha
maadhimisho ya ya miaka 54 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi la wananchi wa
Tanzania sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Polisi Wilayani
Modulo.
Alisema
kuwa niwajibu wa kila mwananchi wa Tanzania anawajibu wakulinda na
kuenzi amani ya nchi yetu kama ilivyo hasisiwa na wazee wetu
waliotutangulia.
Kimanta
aliwapongeza jeshi kwa kazi wanazofanyaupamoja nashighuli mbalimbali
mbalimbali za kijamii wanazozifa,huku akitumia muda huo kupongeza
uongozi wa chuo na wanachuo wa chuo cha mafunzo ya Jeshi Monduli
kwajinsi wanamahusiano mazuri baina yao na wananchi.
Kwa
upande wake kaimu mkuu wa chuo cha mafunzo ya jeshi Monduli Brigedia Je
ne ra li Stephan Justice Mnkande Alisema kuwa maadhimisho hayo
yalianza rasmi August 27nayameitimishwa leo Septemba 1 ambapo alitaja
shughuli zilizofanyika katika maadhimisho hayo kuwa ni Pamoja na usafi
wamazingira yanayozunguka chuo, barabara ya Modulo, njia panda ya Arusha
Dodoma Pamoja na utoaji wa huduma za Afya bure.
Alisema
kuwa hayo yote wamefanya ikiwa ni moja ya mahusiano bora kati ya jamii
na wananchi, alisema kuwa mahusiano mazuri kati ya jamii ya watanzania
ni msingi muhimu katika kudumisha undugu, urafiki na ukaribu
unaoendeleza amani ya nchi yetu.
"napenda
kuwasihi wananchi kwa ujumla kujitaidi kulinda amani yetu kwani
ikipotea ningumu sana kuirejesha, tuendeleeni kuenzi amani yetu "Ali
sema Mnkande.
Aidha
alitaja moja ya mafanikio waliyoyapata tangu kuanzishwa kwa chuo hicho
cha kijeshi miaka 42 iliopita kuwa ni pamoja na kuanzisha kwa kozi ya
shahada ya kwanza ya sayansi ya kijeshi (bachelor Degree in Military
Science) kwa kushirikiana kwa chuo cha uhasibu Arusha (AIA)
iliofunguliwa november 20,2017.
Katika
kilele hichi cha maadhimisho haya pia kulikuwa na michezo mbalimbali
ikiwa nipamoja na maandamano ya kutembea kwa miguu kilometa nne
ilioshirikisha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Monduli, kaimu
mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli, maafisa wa jeshi Monduli, Maafisa
wanafunzi wa chuo cha jeshi Monduli, wanafunzi wa Chuo cha ualimu
Monduli Pamoja na wananchi wa monduli
Aidha pia kulikuwa na michezo mingine kama mpira wa miguu, kukimbiza kuku kuvuta kamba pamoja na mazoezi ya mwili (arabicki
mkuu wawilaya ya Monduli Iddi kimanta akiwa anabadilishana
mawazo na kaimu mkuu wa chuo cha Mafunzo ya kijeshi Monduli Brigedia
Jenerali Stephen Justice Mnkande wakati wa maathimisho ya miaka 54 tangu
kuanzishwa kwa chuo chamafunzo ya kijeshi na miaka 42 tangu kuasisiwa
kwake monduli
kaimu mkuu wa chuo cha mafunzo ya jeshi Monduli Brigedia Je
ne ra li Stephan Justice Mnkande akiongea katika maadhimisho hayo
Mkuu wa wilaya Monduli na kaimu mkuu wa chuo cha kijeshi monduli wakiwa katika matembezi ya kilometa nne