KILIMO CHA MBOGA NA MATUNDA (HORTICULTURE)KINAVYOWEZA KUMTOA MWANAMKE KATIKA UMASKINI

 

NA WOINDE SHIZZA,ARUSHA

 



-   'ushiriki wa wanawake kwenye Kilimo nchini Tanzania kwa takwimu za mwaka 2003 ni asilimia  ni 54%.

-        Kwa ujumla Wanawake asilimia 81% wanafanya shughuli mbalimbali  zinazo husiana na kilimo.

-        Tasnia ya horticulture inayo husisha mazao ya Mbogamboga na matunda ni moja ya sekta ndogo inayo kuwa kwa kasi sana nchini kufikia ukuaji wa asili 8 mpaka 9 kufikia mwaka 2021, huku ikiwa ni sekta inayoingizia mapato serikali kwa wingi kuliko zingine katika sekta ya Kilimo.



Irene Mollel akiendelea kupiga dawa nyanya zake

Irene Mollel ni msichana ambaye ameweza  kujikwamua kiuchumi kupitia  kilimo cha na maua ,mboga,matunda ,mimea itokanayo na mizizi na viungo (horticulture) ,kitu ambacho kilimvutia alipotembelea moja ya maonyesho ya nane nane yaliyowahi kufanyika mkoani Arusha  na sasa  ni mkulima mzuri  na mkubwa wa kilimo cha nyanya.

Alisema kuwa aliaangalia kilimo cha nyanya  ,vitunguu na vingine alipotembelea maonyesho ya nane nane ambapo alivutiwa zaidi alipotembelea banda la  Asasi kilele ya sekta binafsi inayojishughulisha na kuendeleza kilimo cha  horticulture nchini kwa mazao kama maua ,mboga,matunda ,mimea itokanayo na mizizi na viungo TAHA.

Alisema kuwa kabla ya kufika katika maonyesho hayo na kujionea fursa hiyo ya kilimo  alishajaribu kulima lakini hakufanikiwa na alikata tamaa lakini wakati akiendelea kutembelea ,mitandao ya kijamii  na alipofika katika ukurasa  wa kijamii wa asasi ya  Taha  Instagram  aliona tangazo la fursa ya  vijana kusapotiwa na aliamua kujiunga  na kuanza kilimo rasmi.

 

 KUANZA KWAKE  MAFUNZO   RASMI


Irene Mollel alisema kuwa alianza kupata mafunzo kutoka kwa bwana shamba  na alianza kufundishwa kilimo cha matone (drip eligetion system)namna ya  kusia mbegu kwenye vitalu  kwa kutumia treyi ,ambapo  pia alimuandalia ratiba nzuri ya kuweka mbolea ya kisasa aina tofauti tofauti katika nyanya zake  mbali na hili alikuwa akitembelewa na kushauriwa namna ya kusafisha shamba mara kwa mara na mwalimu wake ambaye ni Bwana shamba

Ambapo Bwana shamba huyo kumtembelea katika hatua za mwanzo za kilimo cha nyaya na kumpa ushauri  wa mambo mbalimbali kumemsaidia sana hali iliompelekea   kupata mazao mengi   na yenye ubora.

AMENUFAIKAJE KWA UPANDE WA MASOKO

Anaenda mbali zaidi na  kubainisha kuwa kwa upande wa masoko   amenufaika Kwa sababu ameweza kupewa muongozo kutoka Taha amelima kwa wakati ambao bidhaa inanunulika Kwa bei nzuri ambayo inamuwezesha mkulima

"Kwaiyo wateja wametufata hapa hapa shambani wamenunua kwa bei nzuri  ambayo ni rafiki  kwa mkulima na pia kwa mteja niende ndani zaidi  kipindi  kilichopita  nilipoanza nililima hekari moja lakini sikupata  kitu maana sikuwa na elimu lakini kipindi  kilichofuata nimelima hekari  hiyo hiyo moja nani nimepata mazao mengi ambayo yamenisaidia kuongeza mtaji  wangu wa kilimo" alisema

KIPATO ANACHOKIPATA ANATARAJIA KUFANYIA NINI

Irene anasema kuwa kutokana na kipato anachokipata   kila msimu anapenda kuongeza ekari zingine mbili pamoja na kuongeza idadi ya wafanyakazi  watakao msaidia kufanya  kazi kwa ufanisi zaidi ili aendelee kuwa mfanyabiashara mkubwa zaidi

 ANAWAAMBIA NINI   WATHAMINI WAKE

Aliishukuru sana TAHA pamoja na wania wake kwa kumuwezesha kupata mtaji ,elimu ya kilimo cha horticulture  pamoja na kumfundisha  namna gani ataweza kulima na kupata  fedha  za kuendesha maisha yake

 ANAWAAMBIA NINI WANAWAKE KUHUSIANA NA KILIMO

Irene amewataka wanawake kuacha woga wa Kujiingiza kwenye kilimo ,kwani kilimo cha horticulture ni kizuri na pia kinalipa

Aliwataka wanawake  wale wanaolima kuacha kufanya kilimo cha mazoea   kama vile cha kutegemea mvua badala yake  waingie katika kilimo cha horticulture ambacho unaweza kutumia mbinu mbalimbali  za umwagiliaji wa kisasa.

 Nilipata fursa ya kukutana na mkulima mwingine anaejishughulisha na ulimaji wa zao la Nanasi  aliejitambulisha kwa jina la Eva John  (24) kutoka Kiwangwa Bagamoyo, mkoa wa Pwani ambaye yeye alishidwa kuendelea na masomo  baada ya kumaliza kidato cha nne kutokana na kipato kidogo lakini baada ya hapo hakukata tamaa aliendelea kupambana na kujiingiza katika kilimo cha nanasi .

Anaeleza kuwa alikaa nyumbani kwa kipindi cha muda mrefu  kidogo baada ya hapo akaamua kujiingiza katika kilimo katika shamba lake la ekari 1 mwaka 2018 akiwa na ujuzi mdogo wa uzalishaji na upatikanaji wa masoko uliopelekea  kusababisha mazao kuharibika shambani kutokana na kile kialichodai kukosa masoko ya uhakika

Eva John anaeleza kuwa alianza kulima shamba hilo nakupata hasara hali iliompekea kukata tamaa ya kufanya kilimo hususa ni kilimo hicho cha horticulture lakini  mara baada ya kukutana na wataaalamu wa kilimo hicho na kumpa elimu alianza kuona faida za kilimo hicho na sasa ana shamba la jumla ya ekari sita

Anaeleza kuwa alijiunga na huduma za Tanzania Horticultural Association

 mwanzoni mwa mwaka 2020 na kupitia asasi hiyo Asasi kilele ya Sekta binafsi inayojishughulisha na kukuza kilimo cha Horticulture nchini kinacho husisha maua ,mboga,matunda ,vioungo na mimea itokanayo TAHA amekuwa akipokea ushauri wa kitaalam juu ya mbinu bora za kilimo, upatikanaji wa masoko na usindikaji ili kuongeza thamani ya mazao anayolima pamoja na kudhibiti upotevu wa mazao.

Eva anaenda mbali Zaidi na kubainisha kuwa  soko la  mazao yake  analipata katika  masoko ya Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro na awali  alikuwa akiuza Kenya kabla ya kuzuka kwa Covid - 19.

“Sasa hivi  natarajia kuvuna ekari 5 za mananasi na napia natarajia faida ya zaidi ya shilingi za kitanzania  milioni kumi ( 10), pia kupitia kilimo hichihichi cha horticulture nimeweza kuipatia familia yangu mahitaji ya msingi kama kujenga nyumba yangu  na pia kuwajengea wazazi wangu, nimejenga   fremu za maduka ya kukodisha na naninasaidia wanafunzi 13 kwenye eneo ninaloishi  mahitaji ya shule ili waweze kutimiza ndoto zao na wasiishie njiani kama mimi”

Eva John anawasihi wanawake kutokata tamaa hata kama wamefeli au wameshidwa kuendelea na masomo yao wanaweza wakajiwekeza katika kilimo cha hotculture maana kina lipa na kinafaida kuliko kukaa bila kufanya kazi au kulima kilimo cha mazoea

 MKURUGENZI WA TAHA ALONGA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Asasi kilele ya sekta binafsi inayojishughulisha kuendeleza tasnia ya Horticulture nchini ikijumuisha mazao ya mboga,matunda , maua, viungo na mimea itokanayo na mizizi ya TAHA,  Dkt Jacqueline Mkindi amewataka wanawake kuwa mstari wa mbele kuchangamkia Fursa zinazo tokana na kujihusisha na uzalishaji na mnyororo mzima wa mazao ya horticulture .

Alisema kuwa fursa ni nyingi sana za kilimo cha mazao haya lakini wanawake wengi wamekuwa wakijachwa nyuma  ,na kuacha kuzikimbilia hivyo aliwataka waamke na waanze kuzikimbilia fursa hizi huku akibainisha kuwa masoko yapo ila tatizo kubwa ni uchache wa wanawake wanaoshiriki katika mnyororo mzima wa mazao ya horticulture.

“wanawake wengi wamekuwa wanalalamika ajira  hazipatikani wakati yapo maeneo mengi ya ukezaji ambayo yanaweza kumkomboa mwanamke kiuchumi  na niseme fursa ni nyingi sana za mazao “ Alikazia Dkt. Mkindi.

  Akianisha fursa hizo amesema kuwa wanawake wanaweza kujiunga katika vikundi na kukodi mashamba na kuwa wazalishaji wa mazao kama Nyanya, Vitunguu, Viazi ambayo ni mazao ya muda mfupi na chini ya miongozo ya wataalamu wa TAHA wanaweza kupata mavuno ya kutosha na kupata masoko ya uhakika.

 Licha ya hayo ameongezea kuna fursa zingine ikiwemo kuuza mazao hayo, lakini pia fursa ya kuyaongezea thamani mazao kama ndizi na viazi kwa kusindika.

Mnyororo huu hauishii hapo lakini kuna maeneo kama ya uuzaji wa miche, na kutengeneza bustani za maua mbalimbali ambazo zitawaingizia kipato,

 Akitaja juhudi zinazo fanywa na TAHA kumkwamua mwanamke, Dkt Mkindi  amesema TAHA inatoa elimu ya Kilimo cha kisasa cha Horticulture, elimu ya ujasiriamali kwa wanawake, kuwaunganisha na huduma za mitani na masoko  lakini pia elimu ya lishe na afya bora ambapo wanawake ambao ni zaidi ya asilimia 40 ya wanufaika wa TAHA wameweza kupata elimu hizo.

Aidha aliongeza mazao ya Horticulture kutoka Tanzania yamekua na mwitikio mzuri kutokanna kukua kwa soko katika masoko ya nchi za Afrika Mashariki  pamoja na nchi za kusini mwa Afrika hivyo ni vyema wanawake wakaanza kuwekeza  kwenye kilimo maana kilimo kina lipa .

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

1 Comments:

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia