WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUANDIKA HABARI ZENYE MANUFAA


 Mussa Juma Mkurugenzi Maipac na Mjumbe wa Bodi Misa- tan akitoa nasaha Kwa wahitimu  na wageni  katika chuo cha uandishi wa habari Fanikiwa Arusha yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika chuoni apo kilichopo mbauda ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha

Mjumbe wa Bodi Fanikiwa Journalism School Arusha Elson Makaye kushoto akimkabidhi cheti Cha shukrani mgeni rasmi katika mahafali ya 16 ya chuo hicho  yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika chuo hicho kilichopo Ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha mkoani Arusha

Na Woinde shizza ,Arusha
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuandika habari zenye manufaa Kwa jamii Kwa kuandika habari bunifu zinazolenga kuwakwamua wananchi  kuondokana janga la umaskini.

 Sekta ya habari na utangazaji ikitumika ipasavyo hususani vyombo vya habari mtandaoni kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia  vinaharakisha  zoezi la kuipasha jamii habari kwa wepesi na haraka  zaidi hivyo kuwa chachu ya mabadiliko

 Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya wanahabari inayosaidia jamii za pembezoni nchini MAIPAC,  Musa Juma alisema hayo wakati akihutubia wahitimu na wazazi katika mahafali ya 16 ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Fanikiwa Arusha yaliyofanyika hivi karibuni.

Alisema kuwa ulimwengu wa sasa umekuwa, haswa  katika eneo la sayansi na teknolojia hivyo wana habari wanapaswa kukimbia na ukuaji huo wa teknolojia kwa kuandika habari bora na bunifu pia kuanzisha vyombo vya habari vya mitandaoni ambavyo  vitawasaidia wao kujiajiri.

Hata hivyo ameeleza kuwa  waandishi wengi wanaweza kufungua "Blog, radio mtandao na  Tv za Mitandaoni ambazo  wanaweza kupeleka maudhui mbali mbali ya kihabari na kupitia vyombo hvyo watapatikana wawekezaji mbalimbali ambao wataweka matangazo ya biashara zao ili zionekane na watazamaji au pengine wasomaji.

Musa Juma ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi MISA - TAN na Mkuu wa magazeti ya mwananchii Mkoani Arusha amewataka wahitimu hao wa ngazi ya Stashahada kuzingatia maadili wawapo kazini lakini pia kuwa wabunifu katika kuandika habari za mazingira, kilimo, uchumi, na  mabadiliko ya TABIA NCHI ili kusaidia kuwaweka katika mazingira mazuri zaidi ya kihabari.

Naye mkuu wa chuo hicho Bwana Andrea Ngobole, amewataka wazazi  wa wahitimu    kuwaendeleza zaidi vijana hao katika chuo kikuu ili waendelee kupata elimu zaidi juu ya tasnia ya habari na sekta nyinginezo

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia