Mussa Juma,Babati


Mkuu wa wilaya ya Babati mkoa wa Manyara,Emmanuela Kaganda   amewaaga wanafunzi 40 kutoka shule 4 zilizopo ndani ya eneo la hifadhi ya jamii ya  Wanyamapori ya Burunge(Burunge WMA) kutembelea kujifunza katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Hifadhi ya Ngorongoro.


Ziara ya wanafunzi hao pamoja na.baadhi ya wazazi wao, walimu,maafisa elimu,viongozi wa serikali za vijiji na WMA imeanza leo Desemba 15 na itakamilika Desemba 18 imefadhiliwa na taasisi ya Chemchem Association   iliyowekeza shughuli za Utalii wa picha na hoteli za kitalii katika eneo hilo.


Akizungumza wakati wa kuwaaga wanafunzi hao,Mkuu huyo wa wilaya amesema wanafunzi hao, wanatarajiwa kuwa mabalozi wazuri wa Utalii ma Uhifadhi katika eneo la Burunge WMA.


Kaganda amesema eneo la Burunge WMA ambalo lipo kati kati ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Manyara lina umuhimu mkubwa kwa taifa katika kuendeleza sekta ya Utalii nchini.


"Nyie tunatarajia ndio mtakuwa mabalozi kulilinda eneo hili  ambalo ni mapito ya wanyamapori ili lisiendelee kuvamiwa ,kuharibiwa lakini pia kulihifadhi ili vizazi vijavyo vilikute salama"amesema


Amesema mwasisi wa Taifa la Tanzania Hayati Julius Nyerere, aliamua kuanzishwa hifadhi za Taifa ili kunufaisha watanzania na sasa urithi huo.unatarajiwa kurithishwa vizazi vijavyo.


"Naipongeza sana taasisi ya Chem chem kwa kufadhili safari hii ya mafunzo , mkaone maeneo yaliyohifadhiwa vizuri,muone wanyamapori lakini mjifunze faida za uhifadhi"amesema.


Hata hivyo amesema kimsingi kazi ya kuandaa mabalozi ya Utalii na uhifadhi ilipaswa kufanywa na Viongozi wa Burunge WMA ambao wamekuwa wakipata zaidi ya 1.7 bilioni kwa mwaka kutokana na utalii.


"Naagiza.watoto hawa wakirudi uongozi wa Burunge WMA ukutane nao na kuwaeleza faida za uhifadhi,mapato wanayopata kila mwaka na mgao wa fedha kila kijiji kwa mwaka"amesema


Awali ,Meneja mkuu wa Chem Chem Association Clever Zulu amesema wanafunzi hao wamepatikana baada ya kufanya mitihani ya masuala ya uhifadhi na kufanya vizuri.


Zulu amesema,  Chem Chem inatarajia wanafunzi hao kuwa mabalozi wa Utalii na uhifadhi na wakirejea wawe chachu katika jamii kuendeleza uhifadhi nchini.


"Tumezindua mradi huu mwaka huu na tunatarajia uwe wa kudumu kila mwaka ili kuzalisha mabalozi wengi wa Utalii na Uhifadhi nchini"amesema.


Amesema Tanzania imebahatika kuna na vivutio vingi vya utalii wakiwepo wanyamapori na sasa vinapaswa kulindwa na kuendelezwa kwa wivu mkubwa.


Mwenyekiti wa kijiji cha Sangaiwe,kilichopo ndani ya Burunge WMA, Marian Mwanso  akizungumza katika hafla hiyo,alishukuru chemchem kwa kuwasafirisha watoto na wazazi kwenda kujifunza utalii na uhifadhi.


"Mwekezaji huyo amekuwa na ushirikiano mkubwa na vijiji na sisi Sangaiwe tumenufaika sana na Utalii"amesema

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia