ARUSHA YAKALISHA DUNIA: WAJUMBE 1,500 WA IPU KUMIMINIKA KWA WIKI NZIMA
Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA. Amos Gabriel Makalla mapema leo Alhamisi Disemba 04, 2025 ameupokea na kuzungumza na Ujumbe wa Umoja wa Mabunge duniani (IPU), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano mkubwa wa Mabunge unaotarajiwa kufanyika Mkoani Arusha na kuhusisha Maspika, Wabunge na Viongozi zaidi ya 1500 kutoka kote duniani.
Ujumbe wa IPU umeongozwa na Balozi Ande Filip, akiongozana na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa Geneva,Uswisi Dkt. Hoyce Temu ambapo katika maelezo yake Balozi Ande amesema katika Mkutano huo, Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wa Tanzania.
"Tanzania ni Mwenyeji na sababu kubwa ni ushiriki na historia yake katika IPU na kikubwa zaidi ni namna wao wanavyoiona Tanzania na sisi tumewahakikishia tupo tayari kuwapa ushirikiano kufanikisha mkutano huo mkubwa wa Kihistoria." Amesema Mhe. Makalla.
Makalla amesema Mkutano huo ni fursa kwa Wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla na ukija wakati mzuri katika kudhihirisha amani, usalama na utulivu uliopo nchini na kuaminika kwa Tanzania Kimataifa, akiwataka wananchi kujiandaa kutumia fursa za ujio wa mkutano huo kiuchumi.
Kwa Upande wake Balozi And ite kwaniaba ya Maafisa wengine wa IPU, amesema Mkutano huo wa Kimataifa utafanyika kwa siku sita Jijini Arusha na kulingana na ratiba, washiriki wake kutoka kote duniani watakuwa na zaidi ya siku sita Mkoani Arusha ili kuwapa fursa ya kutembelea maeneo ya kihistoria na Vivutio vya Utalii vilivyopo Arusha na maeneo mengine ya jirani.





0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia