KATIKA KUAZIMISHA SIKUKUU YA SIKU YA AFYA YA MIMEA DUNIANI WATANZANIA WATAKIWA KULINDA NA KUTUNZA AFYA YA MIMEA


  Woinde Shizza ,ARUSHA


 Asilimia 80% ya chakula cha binadamu kinatoka kwenye mimea , asilimia 98% ya oxygen tunayotumia inatoka kwenye mimea lakini mimea hiyo hiyo inakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo kuwepo na visumbufu kama wadudu wahaibifu ,magonjwa pamoja mabadiliko ya tabia nchi kama vile ukame pamoja na uharibifu wa mazingia hali inayosababisha kuwa na upungufu wa chakula pamoja na kuharibika kwa mazingira.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuugenzi mkuu wa (TPHPA )Pro.Joseph Ndunguru ,wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya siku ya afya ya mimea duniani inayofanyika kila mwaka mei 12,ambapo alibainisha kuwa kwa nchi ya Tanzania afya ya mimea ni muhimu sana kwasababu tukiwa na udhibiti wa visupufu mahiri,tutaweza kuongeza tija,ajira na pia kupunguza umasikini na kukuza uchumi wa nchi kwani malighafi ya viwanda yataongezeka kwasababu asilimia 60%ya malighaafi yanayoingia kwenye viwanda yanatokana na sekta ya kilimo

Prof.Ndunguru alisema kuwa kuwepo kwa wadudu wahaibifu magonjwa na mabadiliko ya tabianchi kama vile ukame uchomaji misitu,vinasababisha kupungua kwa chakula hivyo upo umuhimu wa kutunza afya ya mimea ili kufikia malengo.

 Aliongeza kuwa Katika kuadhimisha siku hii Mamlaka ya Afya ya mimea na viuatilifu nchini (TPHPA) imesema kuwa katika mwaka 2022-2023 jumla ya shehena za vipando 189 zilikaguliwa na zilionekana zimekidhi viwango vya matakwa ya afya ya mimea na hivyo kuruhusu biashara kufanyika sambamba na chunguzi za sampuli 103 za mahabara na vitalu nyumba na zilikidhi viwango,ambapo walipokea jumla ya maombi 762 ya vibali vya kuingiza vipando nchini ambapo vibali 756 kwa maana ya 99.2% vilitolewa.

‘’Pia tuliweza kutoa mafunzo kwa wananchi 3100 na maafisa ugani 900katika udhibiti wa mdudu kanitangaze,lakini pia katika kudhibiti viwavijeshi mamlaka ilitoa jumla ya lita za viwatilifu 81563 na kusambazwa katika halmashauri 57 za mikoa ya lindi pwani Morogoro, Geita, Manyara, kilimanjaro,lita 561 za aina mbili niza viwatilifu pia zilisamazwa katika halmashauri ya wilaya ya kilosa,jumla ya wakulima 2987 na maafisa ugani 16 katika halmashauri ya kilombeo walipata mafunzo ya namna ya kudhibiti visumbufu vya mimea,huku ukaguzi wa mazao tani mil 5,343,380 za mazao na nafaka za mizizi mbalimbali mipakani,bandarini na viwanja vya ndege ,jumla vya vyeti 29,033 na usafi wa mimea vilitolewa na kuruhusu biashara ya mazao kufanyika’’

Pia mamlaka iliweza kufanikiwa kudhibiti milipuko ya panya katika kukoa eneo hekari 122190,ili kudhibiti inzi wa matunda jumla ya lita vya viwatilifu 585 na kusambazwa katika wilaya ya mbalimbali ikiwemo muheza,pia tulidhibiti makundi ya kwelea 2,027,000 na kufanikiwa kuokoa hekari1056 ambazo zingekuwa zimeheribiwa,pamoja na kudhibiti nzige na kuokoa jumla ya hekari 195,000,upatikanani wa viwatilifu bora jumla ya viwatilifu vipya 409 na kampuni 198 vilisajiliwa katika kipindi hicho , kuingiza nchini shehena za viwatilifu jumla ya vibali 802 vilitolewa kwa wafanyabishara wa viwatilifu.

 

 


 

“kauli mbiu ya Siku ya afya duniani mwaka huu inasema afya ya mimea kwaajili ya kupunguza umaskini njaa,kulinda mazingiara , kukuza uchumi wanchi zetu ," ambapo alibainisha taasisi yao wanaungana na wenzao duniani kusheherekea siku hii lengo kubwa ni kuhabarisha umma juu ya kutunza afya ya mimea ili tuweze kuyafikia malengo”alisema pro.Ndungu

 


Kwa upaande wake mkuugenzi wa afya ya mimea ambaye pia pia ni afisa mwaandamizi wa utafiti ,ukaguzi wa mimea na afya ya mimea Dr.Benignus Ngowi alisema jukumu la taasisi yao ni kulinda taifa la Tanzania dhidi ya uingiaji wa visumbufu kutoka nje yan chi dhidi ya kusambaa kutoka eneo mmoja la nchi Kwenda eneo lingine la ndani ya nchi hadi nje yan chi na kwa muktadha huo huo Tanzania sio kisiwa jukumu lao lingine ni kuangalia bidhaa ambazo zinazalishwa na kuingizwa kutoka nje yan chi na zinazokwenda nje hazina visumbufu kwa mimea ili kulinda masoko ya ndani yan chi pamoja nanje yan chi.

 


Alibainisha kuwa pia wanafanya kazi ya ukaguzi wa mazao ,mimea ,vipando vyote ambavyo kwa njia moja ama nyingine vinaingizwa Tanzania kwa madhumuni ya kibiashara ,kitafiti,msaada wa aina yeyote ile tunahakikisha havina visumbufu kwa maana havina wadudu waharibifu wa mazao yetu au vimelea vya magonjwa

 


Aliwasihi wananchi hususa ni wafanyabiashara na wakulima iwapo wakitaka kuingiza mazao wapiti katika taasisi yao kupata vibali ili kuepuka usumbufu na kusaidia kuepusha kuingiza vimelea au vidudu viatarishi

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post