Na Woinde Shiza,ARUSHA
VYUO vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi nchi vimetakiwa kuendelee kuhakikisha kwamba elimu ambayo
wanaitoa inalenga katika kumuwezesha
mwanafunzi kuwa na ujuzi ambao
utamfanya aweze kwenda kukabiliana na mazingira anayoishi .
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Joyce Ndalichako alipokuwa
akifungua maonyesho ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi yanayofanyika
mkoani Arusha ambao alisema kuwa maono
na mwelekeo wa serikali ya awamu ya sita
chini ya ouongozi wa DKt. Rais Samia
Suluhu ni kuhakikisha kwamba mitaa
ya elimu inalenga katika
kukuza ujuzi.
“tumeshuhudia katika hizi siku tatu wizara ya
elimu sayansi na teknolojia ilikuwa na kongamano kubwa
,la kuongesha kazi ambayo wameifanya kutekeleza maelekezo ya
Rais aliyoyatoa tarehe 22 april
2021 wakati akihutubia bunge la jamuhuri
ya muungano wa Tanzania na kwenye
sekta ya elimu alisema anataka kuona elimu inajikita zaidi katika kujenga ujuzi
na katika mabanda haya mkipita mtajionea uhalisia sasa wa kile ambacho
Rais wetu alikuwa anakisema na namna
ambavyo sasa vyuo vinaendelea kutekeleza
na kuimarisha mafunzo yao ili
kuhakikisha ujuzi unapewa kipaumbele “alisema
Joyce
Alibainisha kuwa kwa sasa hivi vyuo vimekuwa vikiendelea
kuwafundisha wanafunzi katika
kutatua changamoto katika
mazingira yao ambapo alitolea mfano katika
banda la chuo cha usafirishaji NIT kuna mwanafunzi kutoka kigoma ambaye yeye ameweza kutengeneza
mashine ya kuchakata mazao ya michikichi ambapo alibainisha kuwa
mwanafunzi huyo alisukumwa kutengeneza
mashine hiyo kutokana na jinsi alivyokuwa anaona mama yake anasumbuka kutumia ile mashine ya zamani ambayo mama yake alikuwa anatumia ya kuzungusha miti
kupitia mikono kwa aiyo alivyopata nafasi ya kusoma ndio akaona atengeneze jambo litakaloweza kutatua
tatizo hilo .
Katibu mtendaji baraza la taifa la elimu ya
ufundi na mafunzo a ufundi stadi Dkt Adolf Rutayuga alisema kuwa
maonyesho haya yamekuwa yanafanyika kila mwaka na haya ni maonyesho ya tano na
yanaendana sambamba na kongamano .ambapo alibainisha kuwa wamekuwa wakikutanisha vyuo vilivyopo hapa nchini viwaonyeshe uma wa
watanzania kuwa wanafanya nini ,teknolojia zinazoibuka kule ,mafunzo mbalimbali
yanayotolewa na kuwapa motisha
vijana ambao wanataka kuingia kwenye
mafunzo ya elimu ya ufundi mafunzo ya ufundi stadi wajue
kinachotokea .
Aidha alisema katika maonyesho haya na kongamano wanakutanisha wadau mbalimbali
wa ndani ya nchi nan je ya nchi kukaa
kwa pamoja na kujaribu kujadiliana
kujenga ujuzi ninini na nini kinaitajika
vijana kutoka kwenye elimu hii wakiwa mahiri manake nini ,vyuo
vijiandaje na kozi kazi zinapaswa kufundishwa kwenye dunia ya kazi vinatakiwa
kitu gani ,waajiri waliouthuria
wanaeleza kwamba ni kitu gani kinamapungufu kwenye kufundisha ili vyuo vijue vinajiandaaje ili kuakikisha
kile ambacho wanakifundisha kiweze kujibu mahitaji ambayo yanaitajika katika
soko
Aliwasihi wananchi wajitokeze kutoa maoni yao katika maonyesho hayo ili vyuo viweze kubadilika na kuweza kutoa
mafunzo yanayolenga kuzalisha vijana wanaoweza
kutenda na kuaachana na mambo ya
kuongea tu na watu
wajue kitu kinafanyikaje na waweze hata kuweka bunifu zao ambazo zitasaidia kutatua matatizo yaliopo
katika jamii zetu
Alisema kuwa kunawashiriki Zaidi ya 160 ambao
wanavibanda na kila kibanda ni chuo kinaonyesha kinafanya nini lakini kwa upande
wa kongamano kuna washiriki zaidi ya 300 na wanaendelea kuongezeka maana
wengine wanatoka mbali zaidi .