ZAIDI YA KAMPUNI 300 KUSHIRIKI MAONYESHO YA KARIBU KILL FAIR

 

Afisa mtendaji mkuu wa benki ya CRDB Boma Rabilla alikabidhi hundi ya milioni 50 waandaaji wa maonyesho ya KARIBU KILL FAIR, Dominic Shoo wakwanza kulia na Tom Kunkler wapili kutoka kulia

Na Woinde Shizza, ARUSHA 

 Zaidi ya nchi 30 kutoka Duniani na makampuni zaidi ya 300 zinatarajia kushiriki maonyesho ya Karibu kill fair viwanja vya Magereza kisongo jijini Arusha yanayotarajiwa kufanyika  June 2 hadi nne   mwaka huu wa 2023

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi mtendaji wa kill fair promotion limited Dominic Shoo amesema kuwa maonyesho ya karibu Kili fair yanatumika pia kuuza  nchi yetu ya Tanzania kwasababu wanapotembea  kutafuta masoko nchi zingine duniani  wanatumia pia kuitangaza na kuwasihi watu waje katika maonyesho haya ili  waweze kuona vivutio vilivyopo pamoja na  kuonana na watanzania.

Shoo amesema kuwa ongezeko la utalii nchini Tanzania limechangiwa zaidi na kampuni ya karibu kill fair ambapo amesema  maonyesho haya ni yakimataifa hivyo  yatashirikisha watu mbalimbali kutoka nchi 30  nawanatarajia   kuona Tanzania ina nini ili waweze kuitembelea vivutio vya utalii vinavyo patikana hapa nchini .

Makamu mwenyekiti wa Tato Henry Kimambo amesema kuwa kuwa lengo kubwa la tukio hilo la maonyesho ni kuwezesha kuunganisha wadau wa sekta ya utalii kutoka nchini na nje ya nchi ya Tanzania kupelekea kuungana na mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuweza kufikisha watalii 500 mpaka kufikia mwaka 2025.


"Na ijulikane kuwa katika nchi ya Tanzania benki ya serikali ya crdb siyo mara ya kwanza kudhamini maonesho hayo na kulingana na takwimu kutoka benki kuu nchini mwaka2022 baada ya ya biashara ya dhahabu kuingiza pesa nyingi Tanzania biashara inayofuatia ni hii ya utalii ambapo serikali imeweza kuingiza kiasi cha bilion 2.4 za kimarekani hii inaonesha namna ambavyo serikali inapata mapato"alisema


Afisa mtendaji mkuu wa benki ya CRDB Boma Rabilla  ambao ni miongoni mwa wadhamini katika maonyesho hayo  alisema  kuwa wanajivunia kushiriki katika maonesho hayo kwani lengo la kushiriki ni kulenga kuinua sekta ya utalii,ukizingatia benki ya CRDB kuwa benki ya kwanza nchini kwa kuanzisha kadi maalum ya kuwezesha watalii kufanya malipo wakiwamo wafanyabiashara kunufaika na mikopo mbalimbali ya biashara.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post