mwenyekiti wa Tamida,Sammy Mollel akiongea ofisini kwake
CHAMA cha Wafanyabiashara wa Madini Nchini (TAMIDA), kimeipongeza serikali kwa kurejesha utaratibu wa awali wa madini ya Tanzanite kuuzwa kwenye masoko ya Madini hapa nchini ,tofauti na ilivyokuwa ambapo madini hayo Adimu Duniani yalikuwa yakiuzwa katika Mgodi wa Mererani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara yanakochimbwa.
Mbali na kuruhusu kwa madini hayo ,serikali imerejesha minada ya hadhara ya madini na vito kufanyika baada ya kusimama kwa takribani miaka sita tangu mwaka 2017 na kuagiza mchakato wa taratibu wa biashara hiyo uanze mara moja .
Akiongea na gazeti hili ofisini kwake mwenyekiti wa TAMIDA ,Sammy Mollel, alisema hatua hiyo itasaidia kupanua wigo wa biashara ya madini hayo na hivyo kuongeza pato la taifa kupitia fedha za kigeni kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa wa madini hayo.
"Baada ya serikali kuondoa uuzwaji wa Tanzanite kwenye Masoko ya Madini baadhi ya wauzani wakubwa kutoka nchi mbalimbali duniani waliacha kuja nchini na vijama wengi waliathirika kutokana na kushindwa kumudu safari ya kutoka Arusha kwenda Mererani kufanyabiashara hiyo"
Julai 8,2021 waziri mkuu Kasimu Majaliwa akiwa ziarani katika mji mdogo wa Mererani,mkoani Manyara,aliagiza madini hayo yauzwe Mererani pekee na si mahala pengine popote na kuwataka wafanyabiashara kujenga ofisi Mererani, jambo lililoibua manung'uniko kwa wafanyabiashara wa madini hayo Mkoani Arusha .
Mwenyekiti huyo alisema kuruhusiwa madini hayo kuuzwa katika masoko rasimu ya madini nchini kunatajwa kama mwanzo mpya wa kustawisha uchumi wa taifa kupitia Tanzanite, ambapo wachuuzi Takribani 4000 wa Tanzanite na wafanyabiashara wakubwa zaidi ya 100 waliathirika na uamuazi huo jambo lililotishia kufifisha uchumi wa taifa .
"Ni kweli tumesikia waziri wa madini Doto biteko akieleza bungeni dodoma kuwa amepokea maelekezo kutoka kwa rais Samia kuwa madini ya Tanzanite yaruhusiwe kuuzwa kwenye masoko ya madini na sisi kama wafanyabiashara tumelipokea kwa mikono miwili na tunampongeza sana kwa uamuzi huo"alisema Mollel
Aliongeza kuwa Tamida imejipanga kushirikiana na serikalj katika kuhamasisha kuwekeza katika madini ,na tumejipanga kuhakikisha madini yanayozalishwa na kuthaminishwa kwa ubora unaotakiwa katika soko la dunia.
"Kingine tunachoipongeza serikali ni kurudisha minada na maonesho ya madini na vito ,tumejipanga kwenda kutangaza madini yetu kwa kushirikiana na vyama vingine vya madini duniani"
Alisema wakati Tanzanite ilipoamuriwa kuuzwa Mererani pekee,wafanyabiashara wengi wa madini hayo waliacha kuja nchini kutokana na miundo mbinu iliyopo eneo hilo kutokuwa rafiki na wafanyabiashara hao wakubwa wa madini duniani.
Mollel ambaye alipigania haki hiyo ya Madini ya Tanzanite kuuzwa kwenye masoko rasimi ya madini nchini, alisema serikali ilipoteza mapato mengi kupitia fedha za kigeni kwa wafanyabiashara wakubwa kuacha kuja nchini.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia