TANZIA:ALIEWAHI KUWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA MH.BERNARD MEMBE AFARIKI DUNIA




TANZIA: Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Mhe.Bernard Kamilius Membe, amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Kairuki mkoani Dar es Salaam.


Taarifa za awali zinaeleza kuwa alipata changamoto ya kifua na kupelekwa alfajiri ya leo Hospitalini hapo na baadaye kufariki.




Kwa ufupi. Benard Membe alizaliwa Novemba 9, 1953 katika Kijiji cha Rondo-Chiponda, Wilaya ya Lindi na ni mtoto wa pili kati ya saba wa familia ya Mzee Kamillius Anton Ntanchile na mama Cecilia John Membe. Amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia chama cha Mapinduzi CCM, na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Aidha mwaka 2015 aliwania nafasi ya kuteuliwa kugombea kiti cha urais kupitia CCM ambapo hakufanikiwa na kuhamia chama cha ACT Wazalendo ambako baadaye pia alitoka na kurejea CCM. Mungu aipumzishe roho yake Mahali pema. Amina.


Kwa taarifa zaidi endelea kuwa nasi


#RIPMembe 


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post