A TO Z YAIBUKA MSHINDI WA KIWANDA BORA CHA USALAMA UTUNZAKI WA MAZINGIRA




Kiwanda cha kutengeneza nguo cha jijini Arusha A to Z Textile Mills Limited , kimeibuka na ushindi mzito wa kuwa kiwanda bora cha Usalama na Utunzaji wa Mazingira mahala pa kazi na kushika nafasi ya pili kitaifa .



Akitoa tuzo hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Wenye Ulemavu Mh Prof . Joyce Ndalichako katika zoezi la siku ya Afya na usalama Duniani Kitaifa imefanyika Mjini Morogoro Mgeni Rasmi alikuwa Prof. Ndalichako.


Mh Waziri amekipongeza kiwanda cha Ato Z kwa kutengeneza Mazingira mazuri ya Usalama mahali pa kazi na kujali Mazingira na kutaka viwanda vingine kuheshimu usalama mahala pa kazi na kujali swala zima la Mazingira.



AtoZ ni Miongoni mwa viwanda vikubwa nchini ambavyo ni vinachangia pato pamoja na kulipa kodi kubwa serikalini na ni miongoni mwa viwanda vilivyo ajiri wafanyakazi wengi katika sekta ya viwanda binafsi .



Akipokea Tuzo hiyo Meneja wa Maswala ya Usalama Afya na Mazingira mahala pa kazi,Injinia Harryson Rwehumbiza ambaye amewakilisha Kampuni kwa kuelezea mfumo nzima jinsi ya Kuwalinda wafanyakazi kuepukana na ajali pamoja na magonjwa katika Kiwanda cha A toZ .


Meneja Rwehumbiza amesema kwamba kiwanda hicho kimeonyesha mbinu na mipango endelevu ya kazi katika kudhibiti wafanyakazi wasipate ajali za mara kwa mara kwa kuanzisha semina mbalimbali huku wakisimamiwa na Injinia Harryson Rwehumbiza ndiyo maana A to.Z imeibuka kidedea mshindi wa pili katika sekita ya viwanda vya nguo nchini.



Kiwanda cha ATo Z imekuwa miongoni mwa vinara viwanda ambavyo imeonekana havijakidhi vigezo hivyo Mh waziri amesisitiza kuendelea kujali swala zima la afya kwa wafanyakazi na kuondoa changamoto ambazo zinawakabili wanapokuwa maeneo ya kazi muda wote wawapo kazini huku wakihakikisha wanakuwa na vifaa muhimu vya kufanyia kazi na kutunza Mazingira.



Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post