Wananchi wameshauriwa kutumia bidhaa zenye virutubisho vya asili ili kuweza kujiepusha na maradhi mbalimbali yatokanayo na vyakula ambavyo huweza kusabanisha maradhi mengi.
Hayo yameelezwa na mjasiriamali Tarsila Gervas ambaye ametumia fursa ya mmea uotao baharini wa mwani unaotumika kutibu magonjwa ambapo mmea huo unasemekana kuwa na madini 92 Kati ya madini 102 yanayoitajika mwilini ilikuweza kusaidia kutibu maradhi.
Alisema kuwa kunafaida kutumia viti asilia kwa sababu maisha ambayo watanzania wengi wamekuwa wanaishi kwa sasa wamekuwa wakitumia vitu vinyi sana ambavyo vimekuwa na sumu na wameacha vitu vya asili sana ambapo alisema watanzania wengi wamekuwa wakitumia vitu vya viwandani pamoja na vile ambavyo vina madawa mengi au vimepandwa na madawa mengi ambayo ni sumu.
Alibainisha kuwa kutumia vitu asilia kunafaida kubwa kwani kunasaidia hata kupunguza magonjwa mbalimbali au madhara yatokanayo na madawa (chemical).
"Mmea huu wa mwani tunasema ninasili kwa sababu Kwanza mwenyezi Mungu ameubariki na kuufanya kuwa na madini 92 Kati ya 102 ambayo yanatumika kutibu na kusaidia mwili wa binadamu pia ,bia unaota sehemu ambayo niyaasili baharini hivyo hauwekwi madawa yeyote wakati unavyoota ,naniseme pia ukitumia mwani utakuwa umepata faida nyingi sana katika mwili "alisema
Aidha alitoa wito kwa serikali kusaidia wakulimwa wa zao hili la mwani waweze kizalolisha bidhaa ambayo ni salama na inaweza kutumika kwa matumizi ya binadamu bila kumuadhiri ikiwepo na kuwawekezea nguvu zaidi wale wazalishaji ambao wanazalisha na wapo shambani
"Lakini pia kwa sababu ikitoka shambani lazima iweze kutengenezwa ili iweze kutumika kwa iyo kwa wale ambao tayari wamethubutu na wanauwezo wanaweza wakasaidiwa zaidi kwani kwa sasa naona Rais wetu mpendwa kuna vijana wanawekwa kwenye makundi wanafanya vitu fulani kwa hiyo na hii nayo ikawe ni chachu kwa vijana "alisema Tarsila
Aidha aliwataka vijana kuacha kulala mika kuwa hakuna ajira badala yake wawe wabunifu wajikusanye katika makundi wakae kwa pamoja waanzishe kiwanda chao kidogo ambacho wanaweza kutengeneza mwani na wanaweza kusambaza kwasababu soko lake sio hapa Tanzania tu bali hata nje ya nchi kunasoko kubwa sana na watu wanaitaji na pia wanautumia sana.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia