BREAKING NEWS

Saturday, May 20, 2023

BINTI AELEZA ALIVYOFUKUZWA KWAO ALIPOFAULU SEKONDARI

 Mtoto mwenye umri wa miaka 16 (jina tunalihifadhi)ameeleza adha aliyoipata baada ya kufukuzwa nyumbani kwao na wazazi wake baada ya kufaulu kuingia kidato cha kwanza.


Akizungumza, mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Naishero alisema alilazimika kuishi kwa rafiki zake ambako alitakiwa achangie Sh1,000 kila siku, ili apewe chakula huku akishawishiwa kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na wenyeji wake.


“Nilipofaulu wazazi wangu walinitolea maneno makali, hali iliyonifanya nijihisi vibaya ndio maana hata waliposema niondoke, kweli niliondoka na kwenda kuishi na watu baki.
“Wazazi walisema hawana uwezo wa kunisomesha, nilipokutana na mwalimu aliwahoji kwa nini hawanipeleki shule.

Akizungumza na Mwananchi juzi, mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Naishero alisema alilazimika kuishi kwa rafiki zake ambako alitakiwa achangie Sh1,000 kila siku, ili apewe chakula huku akishawishiwa kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na wenyeji wake.

“Nilipofaulu wazazi wangu walinitolea maneno makali, hali iliyonifanya nijihisi vibaya ndio maana hata waliposema niondoke, kweli niliondoka na kwenda kuishi na watu baki.
“Wazazi walisema hawana uwezo wa kunisomesha, nilipokutana na mwalimu aliwahoji kwa nini hawanipeleki shule.

“Nikiwa kiongozi na mzazi pia niliona kuna umuhimu wa kumsaidia, ili kumuepusha na vishawishi vya marafiki zake waliomtaka achangie pesa ili aweze kuishi katika nyumba yao,” alisema.
Alisema mtoto huyo aliishi kwake kwa siku tano na ndipo wazazi wake walikwenda kuandika maelezo kuwa wako pamoja na mtoto wao, watamsomesha.

“Nikamruhusu arejee ili tusimtenganishe na wazazi na niliwataka watu wa ustawi wa jamii kumuangalia kwa ukaribu mtoto huyo,” alisema.

Hata hivyo, mama mzazi wa mtoto huyo, Singiziwa Ally alikanusha kumfukuza akisema alimtaka aende kwa baba yake mzazi anayeishi mbali na kijiji chao.

“Sisi tulimtaka aende kwa baba yake mzazi kumwambia mahitaji yake, lakini cha ajabu mtoto akaenda kukaa kwa marafiki, hata sisi tulishangaa,” alisema. Akimzungumzia mtoto huyo, mkuu wa Shule ya Sekondari Naishero, Mariam Msanya alisema alimpokea akiwa na barua kutoka ustawi wa jamii, baada ya mahojiano alimuona ni mtoto anayependa shule.

“Huyu mtoto anajitahidi katika masomo, licha ya changamoto anazopitia, anahitaji msaada wa wazazi na jamii,” alisema.

Ofisa ustawi wa jamii wa wilaya hiyo, Johari Rashid alisema shule ilipofunguliwa mtoto huyo alikwenda baada ya kusikia agizo la mkuu wa wilaya kwenda shuleni hata kama hawana sare.

Chanzi:mwananchi

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates