Kuwatetea
Mabinti: Mapambano Dhidi ya Maambukizi ya Ukimwi kwa Wanawake
Wanawake
na wasichana wanaoishi kusini mwa jagwa la Sahara ,ikiwemo nchini Tanzania
wamelemewa na mzigo mkubwa wa ugonjwa wa Ukimwi ,Kwa kiasi kikubwa mzigo huo
unatokana mifumo ya kijinsia ,kijamii,na kiutamaduni pamoja na kukosekana Kwa usawa wa kiuchumi.
UKIMWI
NI NINI?
UKIMWI
Ukosefu Wa Kinga Mwilini ni ugonjwa unaosababishwa na VVU (Virusi Vya UKIMWI)
UKIMWI hudhoofisha mfumo wa kinga za mwili na kumfanya mtu aweze kuambukizwa au
kupata magonjwa mbalimbali.
Wanawake
na wasichana wanaendelea ubeba mzigo
mkubwa wa VVU nchini Kwa mwaka 2018 kulikuwa na WAVIU 1,600,000 wa makundi mbalimbali kati ya wale
wenye miaka 15 na zaidi walikuwemo
wanawake 880,000 ikilinganishwa na WAVIU wanaume mwaka 2018 ,wasichana wenye rika la balehe na wanawake
vijana 54000 wenye umri wa miaka 10-19
walikuwa wanaishi na VVU
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari UNAIDS AIDS info 2019 inaeleza kuwa nchi ya Tanzania
kiwango cha maambukizi ya UKIMWI ni 2.5 kati ya watu wazima 1000 wenye miaka 15-49 tangu mwaka 2010 ,
maambukizi ya VVU yamepungua Kwa asilimia 12 Kwa watu wazima wenye umri zaidi
ya miaka 15 kuanzia 73000 hadi 64000 ya maambukizi mapya na hii ni hatua nzuri lakini pia hatua hii aifikii lengo la
kupunguza maambukizi mapya 18000 hadi
kufikia mwaka 2020.
Kwa
upande wa maambukizi mapya ya VVU bado kunatofauti kubwa ya maambukizi
kulingana na jinsia Kwa mwaka 2018 kulikuwa na maambukizi mapya 36000
miongoni mwa wanawake na
maambukizi mapya 27000 miongoni mwa
wanaume wenye miaka 15 hadi 49
Miongoni
mwa vijana wa rika la balehe wenye miaka 15-19 idadi ya maambukizi mapya Kwa wasichana ni mara tatu zaidi
ikilinganishwa na yale ya wavulana
,kwani kunamaambukizi mapya 8002 Kwa mwaka miongoni mwa wasichana wa
rika la kubalehe mara dufu ya idadi ya
maambukizi mapya (2876) miongoni mwa mapya7986 Kwa mwaka miongoni mwa wale
wenye umri wa miaka 15-24.
VISABABISHI
VIPI VINAVYOCHOCHEA MZIGO WA VVU KWA WASICHANA NA WANAWAKE
Utafiti uliofanywa wa demografia na afya nchini Tanzania mwaka
2019 na shirika la UN Women unaonyesha kuwa wanawake wa nne kati ya 10 wenye
miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili au kingono maishani mwao, ukatili huu wa kingono, kimwili na kisaikolojia
unasababishwa na wenzao ndio aina ya ukatili sana wanawake waliowahi kuolewa
ndoa za utotoni
Kati
ya wasichana watatu mmoja ameolewa kabla
hajafikisha umri wa miaka 18 ndoa za
utotoni zinausishwa na kuanza kifanya ngono mapema ,ngono isiyo salama
,kuongeza hatari ya kufanyiwa ukatilina mwenza wake pamoja na kiwango
kidogo cha elimu
Biashara ya ngono
Mimba
za utotoni huongeza kukosekana Kwa usawa wa kijinsia kikihusishwa na kiwango
cha chini cha elimu na viwango vya kipato ambacho husababisha kuwa kwenye
hatari ya kukosa kipato ambapo
inapelekea kufanyatabia hatarishi ikiwemo kufanya biashara ya ngono
Biashara
ya ngono hufanywa zaidi na wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu waishio mjini
ambao wameshaanza kufanya ngono Kuna sababu mbalimbali zinazomfanya mtu afanye biashara hii baadhi yake ni pamoja
na kuwa katika mazingira magumu ya kiuchumi
na wengine wanajiingiza katika biashara hii Ili kupata maisha bora.
BINTI
ALIEPATA MAAMBUKIZI KUTOKANA NA BIASHARA YA NGONO ALONGA
Naitwa
Fatima mi ni mkazi wa hapa hapa Arusha nilikuwa na fanya biashara hii ya ngono
katika maeneo ya shivas pamoja na maeneo mengine ya mji huu sikuwa najua Kuna mathara makubwa
katika biashara hii.
nawezaje
kukataa pale mwanaume anaponiahidi kunipa fedha zaidi Kwa ajili ya kufanya naye
ngono wakati kitendo cha kumkatalia Kwa lugha rahisi itakuwa ni sawa na kumuudhi?pia
kama mpenzi analalamika na anakataa kutumia kondom ,basi nitamuonea huruma na kukubali kuendelea kufanya naye ngono bila kondomu
Muda
mungine katika biashara hii nilikuwa nikikutana na makashikashi mengi unakuta
unaenda na mwanaume ataki kutumia kondom ,mungine unaenda nae anataka kwanguvu
akuingilie kinyume na maumbile kiukweli
kazi hii ilikuwa ngumu sana na mbaya zaidi nilikuja kupata maambukizi lakini
sijui ninani alienipa ila nashukuru Mungu naendelea vyema Kwa Sasa ningelijua
mapema nisingejihusisha na biashara hii na yote haya niliyafanya kwakuwa
nilikuwa nataka maisha bora mazuri ila mwisho wa siku sijapata nimeambukia
maradhi tu "alisema Fatima
MABINTI NA WANAWAKE WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA ZA NGONO
WASHAURIWA
Mkunga kutoka katika hospitali ya Maternity Afrika
(kivulini hospital) Dkt. Musa Laizer
anaelrza kuwa kunaumuhimu wa
Elimu
na uelewa: Wanawake na mabinti wanahitaji kupata elimu sahihi juu ya Ukimwi,
jinsi unavyosambazwa, na jinsi ya kujilinda, elimu inaweza kujumuisha matumizi
ya kondomu, upimaji wa VVU, na matumizi sahihi ya dawa za kufubaza VVU.
Upatikanaji
wa huduma za afya: Wanawake na mabinti wanapaswa kupata Kwa urahisi wa huduma za afya
zinazohusiana na Ukimwi, ikiwa ni pamoja na kupima VVU, kupata matibabu, na ushauri
nasaha ,ni muhimu kuweka mazingira ambapo wanawake na mabinti wanaweza kutafuta
huduma hizo bila hofu au unyanyapaa.
Kujikinga
dhidi ya unyanyasaji na utumwa wa ngono: Wanawake na mabinti wanahitaji kujua
haki zao na kujifunza jinsi ya kujilinda dhidi ya unyanyasaji na utumwa wa
ngono.,Kupambana na unyanyasaji na kuongeza fursa za kiuchumi kunaweza
kupunguza hatari ya kuambukizwa VVU.
Uwezeshaji
kiuchumi: Kuwapa wanawake na mabinti fursa za kiuchumi inaweza kuwa na athari
chanya kwa afya zao, Kwa kutoa elimu, mafunzo, na mikopo ya biashara, wanawake
na mabinti wanaweza kupata njia mbadala za kujipatia kipato na kuondokana na
hatari zinazohusiana na biashara ya ngono.
Kuelimisha
wanaume na wavulana: Ni muhimu kuwafikia wanaume na wavulana pia, Kuelimisha
juu ya haki sawa, uhusiano mzuri na jinsia, na kuwajibika kwa vitendo vyao
inaweza kusaidia kubadili mtazamo na tabia zinazochangia kuenea kwa Ukimwi.
Kupambana
na unyanyapaa na ubaguzi: Ni muhimu kujenga jamii inayokubali na inayowasaidia
wanawake na mabinti wanaoishi na VVU ,Kuelimisha jamii na kupunguza unyanyapaa
na ubaguzi kunaweza kusaidia wanawake na mabinti kujitambua na kusaidia katika
kupunguza hatari ya kuambukizwa
WITO
KWA SERIKALI
Serikali
inaweza kuchukua hatua kadhaa ili kusaidia wanawake na mabinti kujikinga na
maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Elimu
ya afya na kuelimisha umma: Serikali inaweza kuwekeza katika kampeni za elimu
ya afya na kueneza uelewa kuhusu hatari za maambukizi ya UKIMWI, njia za
kujikinga, na umuhimu wa kupima afya mara kwa mara ,hii inaweza kufanyika
kupitia matangazo ya redio na televisheni, mabango, vijarida, na programu za
elimu katika shule na jamii.
Upatikanaji
wa huduma za afya: Serikali inaweza kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya
kwa wanawake na mabinti, ikiwa ni pamoja na upimaji wa virusi vya UKIMWI,
ushauri nasaha, na matibabu ,Kuwezesha upatikanaji wa huduma hizi kwa gharama
nafuu au bila malipo inaweza kusaidia kupunguza maambukizi na kuwapa wanawake
na mabinti fursa ya kupata matibabu wanayohitaji.
Utoaji
wa kinga za kujilinda: Serikali inaweza kusambaza kinga za kujilinda kama vile
mipira ya kondomu na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya kinga hizo, Kinga za
kujilinda zinaweza kusaidia kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI wakati wa
mahusiano ya kingono.
Kuendeleza
usawa wa kijinsia: Serikali inaweza kuchukua hatua za kukuza usawa wa kijinsia
na kuondoa vikwazo vya kijinsia ambavyo vinaweza kuwafanya wanawake na mabinti
kuwa katika hatari ya kuambukizwa UKIMWI , inaweza kujumuisha kuimarisha sheria
za kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia, kuhakikisha upatikanaji wa elimu
bora kwa wasichana, na kukuza fursa sawa za kiuchumi na kijamii kwa wanawake.
Kusaidia
vikundi vya wanawake na mashirika yasiyo ya kiserikali: Serikali inaweza kutoa
rasilimali na msaada kwa vikundi vya wanawake na mashirika yasiyo ya kiserikali
yanayofanya kazi katika maeneo ya kinga dhidi ya UKIMWI. Hii inaweza kujumuisha
ufadhili wa miradi ya elimu, ushauri nasaha, na huduma za matibabu.