Na Woinde Shizza , ARUSHA
Wabunge wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania na mawakili wa Tanzania wametakiwa kupitia kifungu kwa kifungu sheria inayopelekwa bungeni kwani sheria inakuwa na mambo mengi pamoja na vitu vingi , wasipitishe kiholela ili kuweza kuepuka matatizo mbalimbali yanayoweza kutokea kwa nchi pindi wanapopitisha bila kupitia kwa makini.
Hayo yamebainishwa na mwanasheria ambaye pia ni msimamizi wa masijala ndogo ya mahakama ya Afrika mashariki iliopo jiji Dar es salaam Donald Mafwere wakati akiongea na waandishi wa habari alipoudhuria katika mafunzo ya siku tano ya kuwapatia elimu na ujuzi wa kisheria ambapo wanawafundishwa mafunzo ya uandaaji wa sheria pamoja na uandaaji wa nyaraka za kisheria za serikali ikiwemo juu ya kuandaa mikataba, mafunzo yanayofanyika mkoani Arusha
Alisema kuwa kwa sababu kuna vifungu vingine au mikataba nchi inayoingia ikipitiwa kiholela inaweza kutupeleka au kupeleka nchi katika sehemu ambayo sio sahihi au kuipatia matatizo.
"Mafunzo haya yanaweza kutusaidia kujua ni vitu gani tunaweza kuzingatiwa wakati bunge letu linatunga sheria Kwa sababu tumekuwa tukiona sheria zinatugwa lakini atujui zimepitia mchakato gani ni kinanani wanatunga lakini pia tumejifunza mtu anaepaswa kusimamia maswala ya kuandaa ni mtu wa aina gani na anapaswa kufanya nini wakati anaandaa hizi sheria " alisema Donald
Alibainisha kuwa wamekuwa wakiangalia mikataba mbalimbali iliokuwa inaletwa hapa nchini lakini wanashidwa kujua ubovu wa huo mkataba ulioletwa ni upi nanini kifanywe Ili kuepukana na ubovu wa mikataba mbalimbali ambayo inaweza ikaingiwa baina ya nchi na nchi au kampuni na kampuni ,huku akitoa rai ya kuendelea kutolewa Kwa masoma na vipindi kama hivi kwani vyema viwepo ili waendelee kujua wanapotaka kuandaa sheria na mikataba ni vitu gani viwepo ili kuweza kuepuka matatizo yanayoweza kutokea
Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la wanasheria wa afrika mashariki (East Africa low Society )David Sigano alisema kuwa wameandaa mafunzo ya siku tano ya wanasheria,wabunge na wakili wa kujitegemea kutoka katika chama hicho katika nchi saba za jumuiya hiyo ikiwemo chama cha sheria cha Tanzania ,Kenya ,Rwanda,BurundiBurundi, Zanzibar ,Uganda,chamancha sheria cha Sudan pamoja na nchi zingine za Afrika mashariki wanajishughulisha na maswala ya sheria na wanatoa ushauri kwa serikali zao kuhusu maswala ya kisheria pamoja na maswala ya haki za binadamu na utawala wa kisheria .
Alisema kuwa wamewakusanya mawakili zaidi ya 50 ambao wamewaandalia mafunzo ya uwaandaaji wa maswala ya kisheria pamoja na nyaraka za kisheria wanawafunza jinsi ya kuandaa mikataba pamoja na kuandaa sheria ambazo zitawakilisha watu vizuri na nchi zao vizuri maana wamegundua kwamba kuna wakati sheria zinatugwa lakini zinakuwa na matatizo mahakamani na Kwa mara nyingine zinaonekana hazikuwa makini au watungaji wao hawakuwa makini Kwa hiyo wanawafundisha ili wawe na uwezo wa kuandaa sheria ambazo zinaweza kujisimamia na kutetea wananchi Kwa jinsi inavyofaa.
Aidha aliwataka wanaojihusisha na maswala ya uandaaji wa sheria waweze kuwa makini sababu wanapoandaa sheria zinawakilisha nchi zao ,hivyo waweze kuandaa sheria ambazo zinaumakini.