TAMBUA SABABU ZA WANAWAKE KUTOHUDURIA SOBA HOUSE

 


Tatizo la wanawake wanaotumia na walioathirika na utumiaji wa madawa ya kulevywa (warahibu)kutohudhuria katika nyumba za upataji nafuu ni kubwa mno kutokana na hofu pamoja na kuogopa kunyanyapaliwa.


Licha ya serikali kuendelea kupiga vita matumizi ya dawa za kulevywa nchini ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa watanzania kuacha kutumia dawa hizo iliwemo kupatiwa matibabu katika vituo vya mbalimbali bado wanawake wanaonekana kujiingiza Kwa Kasi huku wengine wakipoteza tumain la kuishi .


Kulingana na takwimu zilizotolewa na mamlaka ya dawa za kulevywa nchini kupitia ofisi ya waziri Mkuu mwaka 2022 inaeleza kuwa idadi ya waraibu walipata huduma katika nyumba za upataji nafuu kuanzia mwaka 2019 hadi mwaka 2022 zinaonyesha kuwa mwaka 2019 wanawake waliopatiwa huduma ni 74 huku wanaume wakiwa 3609 kwaa mwaka 2020 wanawake 160 huku wanaume wakiwa 2103 Kwa mwaka 2021 wanawake 160 wanaume 2949 na Kwa mwaka 2022 wanawake 124 na wanaume 3161 hii inaonyesha ni namna gani muitikio wa wanawake kuhudhuria huduma za upataji nafuu.


ATHARI ZITOKANAZO NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA



Mwanasaikolojia kutoka Serenity gate rehab Edward Mwendamseke anaeleza baadhi za adhari zitokanazo na utumiaji wa dawa za kulevywa kuwa ni pamoja na 

 


Watu wengi wanaojidunga wanajikuta watumiaji kiasi kikubwa cha dawa za kulevya (overdose) wanaweza kufa anakuwa na UWEZEKANO kupata ugonjwa wa 

- saratani

-kukosa usingizi 

-kukosa hamu ya kula na kuoza meno.

- Aidha, matumizi ya dawa zakulevya husababisha ulemavu na upungufu wa kinga ya mwili dhidi ya maradhi.

-Dawaza kulevya kwa wanawake huvuruga mtiriko wa hedhi

 -huharibu mimba 

-husababisha kuzaliwa kwa watoto wenye uraibu wa dawa za kulevya, waliodumaa kaimwili nakiakili

-matatizo ya moyo pamoja na 

 ulemavu wa viungo au kujifungua watoto njiti.


Kwa ujumlamatumizi ya dawa hizi hupunguza umri wa kuishi wa mtumiaji kutokana na maradhi,uhalifu au kuzidisha kiasi cha dawa (overdose).




MATATIZO GANI MARAHIBU HUSABABISHA KATIKA JAMII


Anaenda mbali na kueleza kuwa Waraibu wa dawa za kulevya kwenye jamii husababisha kukithiri kwa vitendo vyakihalifu ikiwemo wizi, ukahaba, utapeli na uporaji kwa ajili ya kupata fedha zakununulia dawa hizo.


 Matumizi ya dawa za kulevya huvuruga mahusiano katika familia na kusababisha kutengana kwa wazazi, kutelekeza familia hivyo watoto kukosa malezi bora na kukimbilia mitaani. 


Pia, matumizi ya dawa za kulevya kwawanafunzi huathiri maendeleo ya mwanafunzi shuleni na kusababisha utoro, utovuwa nidhamu na hata kufukuzwa shule.


Dawa za kulevya huchangia ongezeko la maambukizi ya VVU, homa ya ini na kifuakikuu katika jamii kutoka kwa watumiaji ambao huwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya maradhi hayo. 


Aidha, matumizi ya dawa za kulevya husababisha ajali zinazoweza kuepukika ambazo husababisha ulemavu, vifo, uharibifu wa mali namiundombinu. 


Kiuchumi


Matumizi ya dawa za kulevya hupunguza ufanisi kazini na kusababisha kupoteza ajiraau kufilisika. 


Mtumiaji hushindwa kuajirika hivyo kusababisha umaskini kwake, jamiiyake na Taifa kwa ujumla, Aidha, waraibu wa dawa za kulevya ambao wengi ni vijanahujikuta wakishindwa kujihusisha na shughuli za uzalishaji mali na hupoteza nguvukazi ya Taifa.


KITU GANI SERIKALI WANAFANYA KUWASAIDIA 



Akielezea baadhi ya vitu ambayo serikali inavifanya Kwa warahibu hawa ili kuwasaidia administrator wa kituo cha Serenity gate rehab Elineema Kimaro alisema Serikali huingia gharama zisizo za lazima kwa ajili ya tiba ya waraibu na kutoa elimu ,Aidha matumizi ya dawa za kulevya yanaambatana na uhalifu unaoweza kusababishakufungwa gerezani hivyo, serikali huingia gharama za kuwahudumia wafungwa hao badala ya kuelekeza rasilimali hizo kwenye shughuli za maendeleo.


MWANAMKE ALIETUMIA DAWA ZA KULEVYWA AFUNGUKA


Aisha ni mwanamke mwenye umri wa miaka 32 anaishi mkoani Arusha anasema kuwa yeye alikuwa ni mrahibu wa madawa ya kulevywa  


"Mimi ni mwanamke Sina mtoto na nilianza kutumia dawa za kulevywa kipindi kirefu na marafiki walinisababisha Kwa kunishawishi nianze kutumia, kiukweli awali nilikuwa sioni mathara ya utumiaji madawa haya lakini baadae ndio nilikuja kuona ,siku amua mwenyewe kwenda katika hizi nyumba za uangalizu (rehabu)bali babayangu ndio alinichukuwa Kwa nguvu na kunipeleka soba "


Kiukweli tangu niingie uku nimeona mabadiliko Sasa hivi naweza ata kufanya shughuli zangu binafsi tofauti na zamani nilikuwa sifanyi kazi yeyote"


SABABU GANI ZINAFANYA WANAWAKE WASIENDE KWENYE SOBA HOUSE


Anaeleza kuwa wanawake wengi ni warahibu lakini wamekuwa hawaendi katika vituo vya uangalizi kutokana kihofia kunyanyapaliwa ,kutengwa na wengine aibu ndio imewabana hivyo ndio maana wengi wao hawazubutu kwenda katika nyumba za upataji nafuu 


Anabainisha kuwa Asilimia kubwa ya Wanawake unakuta waneathiriwa na unywaji pombe kupita kiasi ,utumiaji wa bangi ,sigara ,mirungi pamoja na unga .


WITO GANI ANATOA KWA WANAWAKE AMBAO NI WARAHIBU

 

-Wanawake wengi wamekuwa wakuwa ni warahibu lakini wanaogopa kwenda kuanza matibabu lakini aliwasihi kuacha kuogopa na kwenda katika vituo vya upataji nafuu kuanzia matibabu


-Muamko uliopo kwenye jamii kwamba wanawake pia ni warahibu ni mdogo hivyo ni vyema wanawake wakajikubali na kujitoa kwenda kupata huduma.


-Wanawake waache kuogopa kunyanyapaliwa kutokana na mazingira magumu ambayo wanapitia kuacha kuogopa kusemwa vibaya,waache kuogopa kuvuliwa utu wao na pia waache kuogopa kusema Siri zao wakiofia kusemwa vibaya maana Kuna baadhi ya Wanawake wanafanyiwa vitendo vibaya na wanaume zao ikiwemo kulazimishwa kutumia dawa za kulevywa wakati hawataki


-Aliwataka wanawake washauri misikitini au makanisano nawaende na wajitokeze katika vituo wakapewe elimu na ushauri


SERIKALI IFANYE NINI KUSAIDIA WANAWAKE HAWA


-Serikali itoe elimu Kwa wanawake juu ya umuhimu wa kuhuzuria katika nyumba za upataji nafuu


-serikali ianzishe kampeni mbalimbali Kwa ya kuhamasisha wanawake kuacha kuogopa kwenda katika vituo vya upataji nafuu pia kuwaelimisha juu ya mazara ya utumiaji wa madawa ya kulevywa 

 pamoja na pombe kupita kiasi


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post