Nguvu ya Ubunifu: Mwanamke Mfanyabiashara na Mwalimu wa Batiki
Katika ulimwengu wa biashara na
sanaa, kuna wanawake ambao wameinuka na kuvutia umati kwa ujasir, ubunif na uwezo wao wa kufanikisha mambo
makubwa. Mmoja wa
wanawake hao ni Tausi Swalehe, mwanamke mfanyabiashara na mwalimu anayetawala
sanaa ya ubunifu kupitia utengenezaji wa batiki.
Tausi ni jina linaloleta msisimko
katika tasnia ya ubunifu hususa ni katika nyanja ya siasa na fani ya
utengenezaji batiki katika miaka kadhaa, ameweza kusimama imara na kuongoza
katika biashara yake ya utengenezaji wa batiki.
Batiki ni sanaa ya kuchora na kubuni
mitindo kwenye nguo na vitambaa kwa kutumia mbinu maalum. Tausi amejitosa
katika hili kwa moyo wote na kufanikiwa kufanya batiki kuwa sehemu muhimu ya
utamaduni na mitindo ya mavazi.
TAUSI AFUNGUKA
Mimi ni mama ambaye ni mwana
siasa na mfanya biashara ujuzi wangu na uzoefu katika sanaa ya batiki, nimeweza
kuwa mwalimu bora ninayewapa wanawake wengine ujuzi na elimu ya kutengeneza
batiki
Nimewawezesha wanawake kujifunza na
kukuza vipaji vyao katika sanaa hii ya kuvutia Mafunzo yangu yanazingatia
ubunifu, ujasiri, na uhuru wa kujieleza, ambayo ni nguzo muhimu katika sanaa ya
batiki.
MAFANIKIO YAKE YAPOJE?
Mafanikio yangu katika biashara
yanaonekana wazi kupitia ubora na mitindo ya kipekee ya batiki ninayotengeneza
na katika kazi zangu Kila kipande cha batiki kinajulikana kwa ubora wake na
uhalisia wa kazi ya mikono.
Kwa uwezo wangu wa kubuni mitindo ya
kuvutia na kupendeza, nimekuwa chaguo la wateja wengi, iwe ni wabunifu wa
mitindo, wasanii, au watu binafsi wanaotafuta bidhaa za ubunifu na za kipekee.
Licha ya kufanya vizuri katika
biashara yangu , pia nimeweka lengo la kusaidia wanawake wengine
kufanikiwa,ninaamini kuwa ubunifu na biashara zinaweza kuwa chanzo cha uhuru wa
kiuchumi kwa wanawake ,nimekuwa nikihamasisha wanawake kutobweteka na kujifunza
kuwa wajasiriamali wazuri ,ninaamini kuwa wanawake wanapaswa kuwa na uhuru wa
kifedha na kuweza kuchangia katika ukuaji wa ki katika jamii.
Pia nimepata Mafanikio binafsi
kupitia shughuli zangu nimeweza kuendesha familia yangu na kufanya mambo yangu
ya kimaendeleleo ambayo siwezi kuyasema hapa.
ANAWEZA KUFANYA NINI ZAIDI?
Kwa kuwa na sauti yenye nguvu, Tausi
amekuwa msemaji mzuri kwa ajili ya haki na ustawi wa wanawake ametumia umaarufu
wake kuunda mazungumzo na mijadala juu ya maswala yanayowakabili wanawake
katika jamii, ikiwa ni pamoja na usawa wa kijinsia, fursa za ajira, na
upatikanaji wa mikopo na elimu ya biashara.
Anaamini kwamba wanawake wana uwezo
mkubwa wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii, na amekuwa akitoa rai kwa
serikali na taasisi kuweka mazingira rafiki kwa wanawake kufanikiwa.
UTHUBUTU ,UJASIRI NA UWEZO WA
KUFANIKIWA KWAKE
Tausi Swalehe ameonyesha uwezo mkubwa
katika tasnia ya utengenezaji wa batiki, ujuzi wake wa kuchora na kubuni
mitindo ya batiki umewavutia wateja wengi na kumfanya awe maarufu katika sekta
hiyo.,Kwa kujitolea kwake na ubunifu wake, ameweza kukuza biashara yake na
kupewa oda mbalimbali na watu mbalimbali bidhaa zake za batiki zinaonyesha
ubora na umahiri, na hivyo kumfanya awe chaguo la kwanza kwa wateja wengi.
Tofauti na utengenezaji wa batiki,
Tausi amekuwa akitoa huduma ya upishi kwenye sherehe na matukio mbalimbali
pamoja na shughuli za kiserikali ,Ustadi wake katika kupika vyakula mbalimbali
na huduma bora kwa wateja umemfanya awe mmoja wa watoa huduma wanaotafutwa sana
,anaelewa umuhimu wa kutoa huduma ya hali ya juu na kuwafurahisha wateja wake,
na hivyo kuimarisha sifa yake katika tasnia hiyo.
Lakini mafanikio ya Tausi hayako tu
katika biashara zake bali yeye pia ni mwanasiasa anayetumia sauti yake
kuwawakilisha wanawake na kuwasaidia kufikia uwezeshaji wa kiuchumi.
Tausi amejitolea sana katika
kuelimisha na kuhamasisha wanawake wengine, anawashauri wanawake kutobweteka na
hali yao ya sasa, bali badala yake wawe tayari kufanya kazi kwa bidii na
kuthubutu.
Kupitia uzoefu wake katika biashara
na siasa, Tausi ameona changamoto ambazo wanawake wanakabiliana nazo, anatambua
umuhimu wa serikali kuchukua hatua kwa kuwasaidia wanawake kupata mikopo yenye
riba nafuu na elimu ya biashara Aidha anasisitiza umuhimu wa kuwapa wanawake
fursa ya kujiendeleza kiuchumi na kuondokana na utegemezi.
Mafanikio ya Tausi hayajakoma tu
kwenye biashara na siasa.,Yeye pia ni mwalimu ambaye amejitolea kutoa elimu ya
utengenezaji wa batiki na upishi kwa wanawake, Anaelewa umuhimu wa kuelimisha
na kuwapa wanawake ujuzi na maarifa ya kujitegemea anatumia jukwaa lake kama
mwanasiasa na mfanyabiashara kufikisha ujumbe wake na
Tausi Swalehe pia amejitosa katika
uwanja wa siasa na kutumia nafasi yake kuwasemea wanawake na kuwawakilisha
katika maamuzi muhimu, Kupitia sauti yake, ameshauri wanawake kutobweteka na
kufanya kazi kwa bidii.
AWAHASA WANAWAKE WENZAKE
Amewahimiza wanawake kuwa na ujasiri
wa siasa na kutumia nafasi yake kuwasemea wanawake na kuwawakilisha katika
maamuzi muhimu.,Kupitia sauti yake, ameshauri wanawake kutobweteka na kufanya
kazi kwa bidii.
Amewataka wanawake kuwa na ujasiri wa
kuchukua hatua na kushinda changamoto wanazokabiliana nazo ambapo allijitolea
mfano yeye mwenyewe amekuwa na safari ngumu, lakini hajakata tamaa bali
anatumia uzoefu wake kama chanzo cha hamasa kwa wanawake wanawake wengine,
akiwaonyesha kuwa wanaweza kufanya.
Tausi Swalehe amejitolea kusaidia
jamii yake na kuchangia katika maendeleo ya kijamii,ambapo amegundua umuhimu wa
elimu na amekuwa akitilia mkazo suala la elimu kwa watoto.
Mbali na jitihada zake za kielimu,
Tausi Swalehe pia amekuwa akihamasisha juu ya umuhimu wa mazingira safi na
salama, Ameshiriki katika shughuli za usafi wa mazingira na upandaji miti
katika maeneo ya umma,ambapo Ametambua kuwa mazingira safi yanachangia afya
bora na ustawi wa jamii. Kupitia juhudi zake, amewahamasisha wanawake na vijana
kushiriki katika shughuli za kujenga na kutunza mazingira.
Tausi Swalehe amejitahidi sana kuwa
mfano bora kwa wanawake wengine, na amekuwa akiwahamasisha kuchukua hatua na
kufanikiwa katika maisha yao ,Amewahimiza wanawake kujiamini, kujitambua
thamani yao, na kujitahidi kufikia malengo yao.
Yeye mwenyewe ni mfano hai wa
mwanamke aliyejituma na kufanikiwa, na amekuwa akishiriki hadithi yake ya
mafanikio kama chanzo cha hamasa kwa wanawake wengine.
Kwa kumalizia, Tausi Swalehe ni mfano
wa kuigwa katika jamii kama mwanasiasa, mfanyabiashara, na mshawishi wa
wanawake, Ameweza kufanikiwa katika biashara yake, kuwa sauti ya wanawake
katika siasa, na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii yake ,
Juhudi zake zinazolenga elimu,
mazingira, na ujasiriamali zimewawezesha wanawake wengi kupata motisha na
kuweza kufikia malengo yao anaendelea kuwa chanzo cha hamasa na mfano wa kuigwa
kwa kizazi cha sasa na kijacho pia kutokana na kazi zake Ameweza kupata tuzo zaidi ya tatu katika mashindano yajulikanayo kama malkia wa Arusha yanayoandaliwa na phide intatament na yanashirikisha wanawake wa pande mbalimbali za Tanzania