Ukeketaji
Watoto Longido: Wananchi Wapinga Vitendo vya Ukandamizaji
Wakati serikali ikiendelea kupiga vita swala la
ukeketaji kwa mabinti na watoto wa kike Kwa ujumla kumebainika
kuwepo wa matukio ya ukeketaji kwa watoto waliochini ya miaka mitano
wilayani Longido mkoa wa Arusha.
Baadhi
ya wazazi wa Jamii ya kifugaji katika Wilaya hiyo,wameanza kuwakeketa watoto
wakiwa wachanga ili kukwepa kukamatwa na vyombo vya dola.
Wilaya
ya Longido, iliyoko mkoani Arusha nchini Tanzania, imekuwa ikikabiliwa na
tatizo la ukeketaji wa watoto wa kike
kwa muda mrefu lakini pia serikali imekuwa ukitumia nguvu kubwa sana kukomesha
tatizo hilo kama sio kulimaliza kabisa
UKEKETAJI
NINI?
Ukeketaji,
ambao pia hujulikana kama ni mchakato
ambao sehemu za kijinsia za wanawake na mabinti hukatwa au kuharibiwa kwa
sababu za kitamaduni, kidini au kijamii.
Ukeketaji
ni mila potofu na vitendo vya ukatili ambavyo havina msingi wowote wa kiafya na
ni kinyume cha haki za binadamu.
Ingawa
kuna sheria inayokataza ukeketaji, bado
vitendo hivyo vinaendelea katika maeneo mengi, hasa katika jamii za vijijini,
Asilimia ya wanawake na mabinti waliokeketwa inatofautiana kulingana na eneo,
kabila, na tamaduni za kikabila.
KIPI
KINACHOPELEKEA UKEKETAJI KUFANYIKA
Mila
potofu pamoja na tamaduni ndio zinazopelekea
baadhi ya wazazi kuwakeketa watoto wao au mabinti wao japo kuwa
kuna baadhi ya wasichana ambao wameelimika na wameamua
kuachana na mila hizo potofu lakini bado kuna baadhi yao wanaendeleza
mila hizo mbaya zaidi wamekuwa wanawakeketa watoto wadogo ambao hawajitambui
Hata
hivyo, wananchi wa Longido wamejitokeza kwa wingi kupinga vitendo hivi vya
ukatili na kusimama imara katika kukabiliana na tatizo hili.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi juu ya
kuibuka matukio ya ukeketaji watoto, Wilaya ya Longido mkoa wa Arusha,
baadhi ya wazazi na maafisa wa serikali wilaya ya Longido walisema bila hatua
kali kuendelea kuchukuliwa ukatili huu dhidi ya watoto hautakoma.
Baadhi
ya wakazi wa Wilaya hiyo ambayo asilimia 95 ya wakazi ni wafugaji wa Jamii
kimasai wameeleza kuwa kutokana na jitihada na serikali wilaya Longido kudhibiti
watoto wakiwa shuleni kufanyiwa ukeketaji baadhi ya wazazi sasa wanakeketa
watoto wachanga.
MWANANCHI
ALONGA
Paulo
Orkediaye mkazi wa Kijiji Cha Oltepesi anasema licha ya elimu kuendelea
kutolewa baadhi ya wazazi wanakeketa watoto wachanga kwa Siri.
"Hi
tabia ni mbaya Sana tunatoa elimu kupinga ukeketaji lakini baadhi ya wazazi
wanaendelea kukeketa mbaya zaidi wanakeketa watoto wadogo ambao awajitambui na
awana ueewa" alisema
Neema
Nailom mkazi wa Olbomba alisema mkakati wa kukeketa watoto wachanga unafanywa
kwa uficho baina ya mama mzazi na baadhi ya Ngariba.
"Huwezi
kubaini mapema kwani ni Siri wanafanya sisi tunawabaini watoto pale ambapo
wanaumwa na kupelekwa Hospitali"alisema
SHUHUDA WA UKEKETAJI AONGEA
Jane
Melei mkazi wa Kimokowa alisema mzazi wake alimkeketa mdogo wake akiwa mdogo
kutokana na Mila hiyo kuendelea na kutaka mtoto awe na heshima ya kuolewa.
"Hata
Mimi nimekeketwa nikiwa mdogo lakini wazazi walifanya hivi ili niwe na hadhi ya
kuolewa maana huku kwetu Kama hujakeketwa ni ngumu kupata mtu wa
kukuoa"alisema.
Merkinoi
Orkendiaye alisema vitendo vya ukeketaji vimekuwa vikiendelea licha ya madhara
ikiwepo kuugua ugonjwa wa festula.
"Mimi
nilifanyiwa ukeketaji nikapata festula na Sasa nimekuwa natoa elimu kupinga ukeketaji"alisema
KIONGOZI
WA SERIKALI AFUNGUKA
Afisa
Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Longido, Grace Mghase amesema kuendelea kwa
vitendo vya ukeketaji vinachangiwa na vijana kuwa wazito kuoa binti ambaye
hajakeketwa.
"Hili
Jambo bado linamizizi Sana sisi tunatoa elimu lakini ajabu kuna vijana na
wasichana wenye elimu lakini bado wanaunga mkono ukeketaji"alone
Grace
alisema hata baadhi ya wanasiasa katika Wilaya hiyo bado wanaogopa Mila hii
potofu kuipinga hadharani.
"Ni
kweli tunataarifa wanakeketa watoto wachanga ili kukwepa kukamatwa lakini
wajuwe serikali ina mkono mrefu tukiwabaini watakamatwa"alisema
MUELIMISHAJI
JAMII AFUNGUKA
Mary
Laizer muelimisha Jamii kupinga ukeketaji Wilaya ya Longido alisema madhara ya
ukeketaji ni makubwa ikiwepo kupoteza maisha.
"Mimi
mwenyewe nilifanyiwa ukeketaji wazazi wangu Walikuwa hawajuwi athari zake
lakini Sasa wamejua na Mimi nimekuwa natoa elimu kupinga ukeketaji"alisema
hivi Sasa wanahamasisha kuwavusha Rika watoto
wa kike bila kuwakeketa lakini pia kutoa elimu kwa vijana kuacha Mila ya
kupinga kuoa msichana ambaye hajakeketwa.
ASASI
ZISIZO ZA KISERIKALI WANENA
Mkurugenzi
wa taasisi ya Ewang'ani Maasai Foundation,Nangidare Laizer alisema changamoto
ya ukeketaji ni kubwa lakini wanaendelea kutoa elimu .
"Mimi
Kama msichana tunakwenda vijiji tunatoa elimu japo kuna wazazi wanaendelea
kukeketa watoto kwa Siri"alisema
Mkurugenzi
wa Shirika la TEMBO la Wilaya ya Longido mkoa Arusha, Pauline Sumayani alisema
changamoto ya ukeketaji bado ipo lakini shirika lao linajitahidi kutoa elimu
kupinga ukeketaji.
"Tunatoa
elimu kwa wanawake,vijana na wazee kuacha ukeketaji na tumekuwa tukitoa zawadi
kwa wazazi ambao wanawavusha Rika watoto bila kuwakeketa"alisema
NINI
KIFANYIKE KUTOKOMEZA UKEKETAJI HUSUSA NI
HUU ULIOIBUKA WA WATOTO
Elimu inahitajika ya kupinga
ukeketaji na elimu inapaswa kuwalenga hata vijana ambao ndio wanachochea
ukeketaji kwa kukataa kuwaoa wasichana ambao hawajakeketwa.
Kutokana
na kuwepo kwa kitendo cha
watoto wachanga kufanyiwa ukeketaji ni vymema serikali kupitia maafisa wa afya kufanya
uchuguzi kwa watoto wanaofikishwa hospital na wakibaini kufanyiwa ukatili
wazazi wachukuliwe hatua.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia