Na Woinde Shizza ARUSHA
Naibu Waziri wa Maji,Mhandisi Maryprisca Mahundi. amesisitiza wakandarasi waliosaini mradi wa sh, bilioni 7.282 kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ili kuwezesha wananchi wapate maji ikiwemo kuwatua ndoo kichwani wanawake na wananchi kwa ujumla.
Muhandisi Mahundi alitoa ombi hilo leo Jijini Arusha kwenye halfa ya utiaji saini mikataba minne ya ujenzi wa miradi ya maji vijijini.
Alisema miradi hiyo ni lazima ikamilike kwa wakati na serikali inauwezo wa kutumia wazawa katika kufanikisha hatua mbalimbali za miradi ya maji hususan ya vipuri.
"Tunampongeza Rais Samia kwa miradi mikubwa anayofanya ikiwemo suala la bandari lakini tutahakikisha hatumkwamishi tunasambaza maji ili kupeleka maendeleo kwa wananchi"
Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella
alisema serikali ya awamu ya sita inafanya mambo mbalimbali ya kuleta maendeleo Mkoani Arusha na kusisitiza kuwa serikali inasimamia zaidi maslahi mapana ya watanzania
Miradi hiyo minne yenye thamani ya sh,bilioni 7.282 inatekelezwa maeneo manne ambayo ni mradi wa maji
ambapo utekelezaji wa mikataba hiyo itakayohudumia watu zaidi ya 54,000 watanufaika .
Huku Mkandarasi mshauri wa kampuni ya Bene Consult (T)LTD ,mhandisi Bernard Msacky ameishukuru serikali kwa kuwaamini na kuahidi kuifanya kadri ya utaalam wao ulivyo katika kuhakikisha wananchi wanapata maji huku mwakilishi wa kampuni ya Jandu,Nitu Jandu alisema nafasi walizopewa watazifanyia kazi ili kuhakikisha wanakamilisha kazi kwa wakati.
Naye mkandarasi wa kampuni ya Climax Unit LTD,Ahamed Kijuu anayetekeleza mradi wa maboresho ya Maji wilayani Karatu , aliishukuru serikali kwa kuwatumia wakandarasi wazawa katika kutekeleza miradi hiyo na hivyo kuondoa dhana kwamba wakandarasi wa kigeni pekee ndo wenye uwezo.
Alisema awali kulikuwa na dhana kwamba wakandarasi wa ndani hawana uwezo wala vitendea kazi vya kufanya kazi ila anashukuru serikali kwa kuona umuhimu wao na kuwapatia kazi.
Kijuu ambaye anatekeleza mradi wa bilioni 1 kwa mkataba wa mwaka mmoja katika vijiji vya Matala na Endonyawet wilayani Karatu aliahidi kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa na kwa kuzingatia muda ukiopangwa.
Naye mkandarasi wa kampuni ya Jandu Plumber ,Ajmer Jandu anayetekeleza mradi wa bilioni 3 katika pori Tengefu la Pololeti awamu ya pili wilayani Ngorongoro. Alishukuru kwa kupata fursa hiyo na kuahidi kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na weledi mkubwa na kwa kuzingatia muda wa mkataba.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia