Ticker

6/recent/ticker-posts

TAMASHA LA WANAWAKE NA UTALII KUFANYIKA NOVEMBER 17 JIJINI ARUSHA ,WANAWAKE WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUJUA FURSA ZA UTALII ZINAZOPATIKANA KATIKA HIFADHI ZETU

 

 mwenyekiti wa Tamasha  lijulikanalo Kwa jina la wanawake na Utalii festival Nangasu Werema akiwaonyesha  waandishi wa habari tuzo ambayo Rais Samia Suluhu ameishinda baada ya filamu yake ya Royal  Tour kuonyeshwa nchini India  ambapo mara baada ya kushinda mwenyekiti  huyo alikabidhiwa Kwa ajili ya kumletea  Rais

Mkurugenzi wa Kampuni ya Sanaa Sana Desgin LTD kampuni ambayo inayohusisha wanawake wenye ulemavu Iren Filex akiongea na waandishi wa habari juu ya vitu watakavyovionyesha katika Tamasha hilo la wanawake na Utalii festival 

mwenyekiti wa Tamasha lijulikanalo Kwa jina la wanawake na Utalii festival Nangasu Werema akiongea na waandishi wa habari juu ya Tamasha la wanawake linalotarajiwa kufanyika novemba 17 katika kituo cha mikutano cha AICC  Tamasha lijulikanalo kama wanawake na Utalii festival uku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa waziri wa maliasili na Utalii 

Na Rose Jackson,Arusha

Waziri wa Mali asili na utalii Anjela Kairuki anatarajiwa kufungua tamasha la Wanawake festival litakalofanyika November 17 jijini Arusha ambalo litalenga kuwezesha kufikia idadi ya watalii milioni Tano ifikapo mwaka 2025

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha mwenyekiti wa tamasha hilo  Nengasu Werema amesema kuwa wameamua kuunga serikali mkono katika jitiada za kutangaza utalii.

Alisema kuwa wao kama wanawake watafanya tamasha hilo ambalo litashirikisha wanawake na wadau wa utalii kwa pamoja ili Wanawake waweze kushiriki kwenye sekta ya utalii.

"Tunataka kutangaza na kukuza sekta ya utalii kwani mada kubwa ya festival hii ni kuangalia namna ambavyo Wanawake wanaweza kujihusisha katika sekta ya utalii ambayo itawezesha kukua kwa uchumi wa Tanzania na wa mtu mmoja mmoja"aliongeza.

Aliongeza kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na tuzo mbali mbali ambazo zitatolewa kwa Wanawake vinara wa utalii lakini pia wataweza kutembekea vivutio vya utalii ikiwemo ya hifadhi ya taifa ngorongoro na na hifadhi ya tarangire.

Kwa upande wake afisa uhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa tarangire Jully Bede aliwapongeza Wanawake hao kwa kuandaa tamasha hilo na kuhaidi kuwapa ushirikiano ikiwemo kuwaeleza Wanawake fursa zilizopo kwenye hifadhi.

Naye mkurugenzi wa Wanawake na utalii Mercy Michae alisema kuwa lengo la wao kuandaa tamasha hilo ambalo litashirikisha wanawake walioko kwenye sekta ya utalii ni  kuhamasisha Wanawake kuunga mkono sekta ya utalii  kuwekeza katika sekta hiyo na hatimae kuweza kuongeza pato la taifa

Post a Comment

0 Comments