Kileo Aonya: "Uhalifu wa Mtandaoni Unazidi Kuigharimu Dunia Trilioni 10.5 kwa Mwaka


Yusuph Kileo, mtaalamu wa usalama wa mtandao na uchunguzi wa makosa ya kimtandao akiongea na waandishi wa habari


Na Woinde Shizza , Arusha 

Katika dunia ya sasa ya teknolojia, uhalifu wa mtandaoni unazidi kushika kasi  Tanzania haijabaki nyuma katika kupambana na changamoto hiyo ,Kupitia jukwaa la nne la Usalama Mtandaoni lililofanyika jijini Arusha, wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi wamekutana kujadili namna ya kujilinda dhidi ya uhalifu wa kidijitali unaozidi kuathiri maisha ya watu na uchumi wa mataifa.

Mmoja wa waliotoa mada katika jukwaa hilo ni Yusuph Kileo, mtaalamu wa usalama wa mtandao na uchunguzi wa makosa ya kimtandao  Katika mchango wake, Kileo alisema moja kwa moja kwamba uhalifu wa mtandaoni sasa unagharimu dunia zaidi ya dola trilioni 10.5 kila mwaka.

 “Hili si jambo la kupuuzia Wizi wa taarifa binafsi, fedha na hata kuvuruga mifumo ya afya, elimu na serikali, yote ni sehemu ya tatizo hili.”

Kileo aliwasilisha mada kuhusu intelijensia ya uhalifu wa kimtandao  akieleza sababu zinazochangia ongezeko lake na mbinu mbalimbali za kulikabili. 

Alisisitiza kuwa vita dhidi ya uhalifu huu si ya serikali peke yake, bali inahitaji ushirikiano wa kila mmoja wetu  kuanzia sekta binafsi, taasisi za elimu, hadi wananchi wa kawaida.

Jukwaa hilo limekusanya wadau kutoka sekta mbalimbali serikali, mashirika binafsi, vyuo vikuu, mashirika ya kiraia na washirika wa kimataifa Wote walijadili kwa kina namna bora ya kulinda taarifa, fedha, na miundombinu ya taifa dhidi ya wahalifu wa kidijitali.

Mbali na mada ya Kileo, mijadala mingine pia imeonesha kuwa kuna haja kubwa ya kuongeza elimu kwa umma kuhusu usalama mtandaoni  hasa kwa vijana wanaotumia intaneti kila siku.

Kwa ujumla, jukwaa hili limeonesha kuwa Tanzania iko tayari kuchukua hatua madhubuti kulinda raia wake dhidi ya vitisho vya kisasa Na kwa mchango wa wataalamu kama Kileo, taifa linaongeza nguvu mpya katika kulinda anga la kidijitali kwa usalama na maendeleo ya wote.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post