Mchimbaji madini na mmiliki wa kampuni ya Tan Youth Tanzanite
Mining,Alhaji Mohamed Karia akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini
ya Tanzanite wa wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara baada ya wachimbaji
hao kumteua kampuni yake iwape huduma ya kuwauzia zana za milipuko kwa
bei nafuu ili kuongeza tija ya uchimbaji
WACHIMBAJI wadogo wa madini ya Tanzanite ya mji mdogo wa Mirerani
Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,wameichagua kampuni ya Tan Youth
Tanzanite Mining ili iwasambazie na kuwauzia zana za milipuko kwa bei
nafuu.
Wameiteua kampuni hiyo baada ya kampuni moja inayotoa huduma hiyo
kuwauzia wachimbaji hao zana za milipuko kwa bei ya juu hivyo
kukwamisha jitihada zao za kuweza kuchimba na kupata madini.
Akizungumza juzi na wachimbaji hao baada ya kampuni yake ya Tan Youth
Tanzanite kuchaguliwa kutoa huduma hiyo Mkurugenzi wake Alhaji Mohamed
Karia alisema ana lengo la kuwasaidia wachimbaji na siyo
kufanyabiashara.
Alhaji Karia alisema yeye ni mchimbaji wa madini ya Tanzanite hivyo
atatumia fursa hiyo ya kufuatilia zana hizo za milipuko ili
kuhakikisha zana hizo zinapatikana kwa wakati na kwa bei nafuu.
“Kama nilivyosema lengo langu ni kuchimba na kusaidia wachimbaji
wadogo na siyo kufanya biashara na nitakwenda India kuonana na Balozi
wetu ili kampuni inayotengeneza zana itueleze kwa nini kuna urasimu,”
alisema Alhaji Karia.
Wachimbaji hao waliazimia kuunga mkono suala hilo kwa kuorodhesha
majina yao na nakala za leseni zao ndani ya wiki moja mpaka mbili ili
kibali cha kampuni hiyo cha kuagiza zana za milipuko kiweze kutolewa
mara moja.
Naye,Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini wadogo wa mkoa wa
Manyara (MAREMA) Zephania Mungaya alisema kupitia kampuni hiyo ya
Alhaji Karia wachimbaji wadogo watafaidika na kuweza kupata zana za
milipuko kwa njia rahisi.
“Tumuunge mkono ndugu yetu Karia ili aweze kufanikisha jambo hili
litakalotuwezesha kupata zana za milipuko kwa bei nafuu na sisi
kuendelea kuchimba madini yetu ya Tanzanite,” alisema Mungaya.
Kwa upande wake,Katibu wa MAREMA,Abubakary Mollel alisema kampuni
ambayo hivi sasa inasambaza na kuwauzia zana za milipuko wachimbaji
wadogo imekuwa inafanya hivyo kwa kupendelea kampuni kubwa.
“Ile kampuni inafanya biashara kwa faida kwani sisi wachimbaji wadogo
tumekuwa tukiuziwa mafuta ya baruti kwa sh130,000 na wachimbaji
wakubwa wanauziwa kwa sh90,000” alisema Mollel.