LUCY STEPHANO ANYAKUWA TAJI LA REDS MISS MBULU

katikati anayepunga mkono ndio mshindi wa redds Miss Mbulu ,Lucy
Stephano (19),kushoto ni mshindi N0.2 ModestaRobert (21) na kulia ni
mshindi N0.3 PascalinaSultan (19) ambaye pia ndio mshindi wa Reds
Miss Talent.
Warembo tisa walioshiriki shindano la kugombea Redds Miss Mbulu mkoani
Manyara wakiwa jukwaani wakishiriki shindano hilo lililofanyika
mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Mbulu.




MREMBO Lucy Stephano (19) wa Tarafa ya Haydom amefanikiwa kushinda
kinyanganyiro cha kuwa mnyange wa Redds Miss Mbulu Mkoani Manyara na
kujinyakulia zawadi ya jiko la gesi na mtungi wenye thamani ya sh
340,000.

Akitangaza matokeo ya ushindi yaliyofanyika katika ukumbi wa Maendeleo
ya Jamii Mbulu,Isaac Masesa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli
hiyo alimtaja mshindi namba mbili ni Modesta Robert (21)
aliyejinyakulia zawadi ya dinner set pamoja na simu ya mkononi aina ya
nikia vyote vikiwa na thamani ya sh.200,000,.

Masesa alimtaja mshindi wa tatu kuwa ni Pascalina Sulsan (19) ambaye
pia alijishindia  ubunifu na kuwa miss Talent ambapo alijinyakulia
kitita cha sh.80,000 pamoja na seti moja ya hotpot.

Masesa alisema mashindano ya kutafuta warembo siyo uhuni kama
wanavyofahamu wengine,bali wametakiwa kutambua kuwa ni kazi kama kazi
nyingine na mbio za urembo ndiyo zimeanza ngazi ya Wilaya  hadi Taifa.

Aliwapongeza wasichana hao kwa kuwa waajasiri na kuhakikisha
wanashinda na kuweza kujinyakulia zawadi mbalimbali kwani kufanya
hivyo kutawasaidia kuongeza sifa mbali mbali katika maisha yao na
kuwataka wajitahidi ili kuweza kushinda mkoani mara
watakaposhindanishwa Juni 2 mwaka huu.

Naye meneja wa mashindano hayo Ofisa Maendeleo ya Wilaya hiyo ya
Mbulu,Harri Sinjela alisema waliojitokeza katika kinyan’ganyilo hicho
ni washiriki tisa na washindi watatu watawakilisha mkoa huo.

Sinjela alisema  wilaya ya Mbulu ina wasichana wengi wenye vigezo
vinavyokidhi kushirikia isipokuwa wamekuwa waoga katika
kuthubutu,jambo ambalo lingeweza kuwafikisha mbali na kuwa Redss
MissTanzania.

“Tunataka Redds miss Tanzania atoke mbulu,kwani kinachoshindikana ni
nini ,ukiangalia wasichana wengi wa huku wana vigezo ninavyotosheleza
kabisa tatizo ni kukosa ujasiri wa kuthubutu,lazima kwenye mashindano
kama haya ujasiri wa kuthubutu unatakiwa kwa kiasi kikubwa,” alisema
Sinjela.

Akizungumzia waliodhamini shindano hilo Sinjela alisema kuwa ni pamoja
na kampuni ya bia Tanzania  kupitia kinywaji chake cha redds,Sanu
parking lodge,New nice cafe na Mama Angel salon,pamoja na libeneke la kaskazini


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post