ICTR YAHITIMISHA KUPOKEA USHAHIDI MAALUM KATIKA KESI YA BIZIMANA
Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya
Rwanda (ICTR) Jumatatu ilihitimisha upokeaji wa ushahidi maalum katika
kesi inayomkabili mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ambaye bado anasakwa na
mahakama hiyo, Augustin Bizimana, Waziri wa zamani wa Ulinzi wa Rwanda.
‘’Naomba
niwajulishe kwamba upokeaji wa ushahidi maalum katika kesi ya Bizimana
uliendelea leo (Jumatatu) asubuhi kwa kupata ushahidi kutoka kwa shahidi
wa mwisho ambaye pia amehitimisha ushahidi wake leo.Hivyo basi kufuatia
hatua hiyo, upokeaji ushahidi huo umehitimishwa,’’ alieleza Msemaji wa
ICTR, Roland Amossouga.
Bizimana
anashitakiwa kwa makosa ya mauaji ya kimbari, kula njama kutenda makosa
hayo, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.
Kesi
nyingine mbili za aina hiyo ambazo ushahidi wake umeshapokelewa ni
pamoja na ile ya mtuhumiwa anayesakwa vikali na anayesadikiwa kuwa ndiyo
mfadhili wa mauaji ya kimbari, Felicien Kabuga na Protais Mpiranya,
aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Walinzi wa Rais.
Utaratibu
wa kupokea ushahidi katika kesi ya mshitakiwa ambaye bado hajakamatwa
umewekwa ili kuhifadhi ushahidi husika uweze kutumika pindi mshitakiwa
akitiwa mbaroni hapo baadaye.
Wakili
wa Zamu wa Bizimana, Yitiha Simbeye aliita jumla ya mashahidi watatu
kwa ajili ya utetezi wa mteja wake. Utetezi katika kesi ya Biziamana
ulianza Mei 14, 2012.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia