WILAYA YA HAI YAITAJI ZAIDI YA TANI 40,000 ZA CHAKULA
Wilaya ya hai inatiaji zaidi ya tani 40,000 za chakula ili
kuweza kukabiliana na upungufu mkubwa wa chakula ulioikumba wilaya
hiyo.
Hayo yalisemwa na mkuu wa wilaya hiyo muheshimiwa Novatus Makunga wakati alipokuwa katika ziara ya mikutano katika vijiji na kata ya masama kusini na masama weruweru .
Hayo yalisemwa na mkuu wa wilaya hiyo muheshimiwa Novatus Makunga wakati alipokuwa katika ziara ya mikutano katika vijiji na kata ya masama kusini na masama weruweru .
Alisema kuwa hali ya chakula imekuwa mbaya sana kwani zaidi ya watu 112,350 wanahitaji msaada wa haraka sana ili kukabiliana na upungufu mkubwa sana wa chakula katika wilaya hiyo.
''kweli hali ya chakula katika vijiji hivi ni mbaya sana kwaani watu hawana chakula na tusipo angalia na kuchukuwa hatua za araka basi tunaweza kupata maafa makubwa kwa wananchi hawa"alisema makunga
Mkuu huyo alifafanua kwamba hali hii ya upungufu wa chakula imeokana na wilaya hiyo kukosa mvua kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo na kusababisha ukosefu wa mavuno hali iliyopelekea wananchi kukosa chakula
Makunga alitaja vijiji vilivyoathirika na janga hilo kuwa ni vya kata ya machame chini ,machame kusini pamoja na machame weruweru.
Aidha aliongeza kuwa maeneo mengini ni ya kata za machame mashariki ,masama ndungai na machame Naarumu ambapo kata zote hizo zimekubwa na katika wilaya hiyo inakadiriwa kuwa na watu wapatao 230,450 .
kwa wa mmoja wa wananchi hao ambae alijitambulisha kwa jina la Ibrahimu swai alisema kuwa wamekuwa wakipata tabu sana kwani mavuno hawana kutokana na mvua kutonyesha kwa wakati kama walivyo zoea.
alisema kuwa wanahofia kukubwa na njaa kwani hawana chakula hivyo wanaimba serekali iwasaidie haraka iwezekanavyo ili kujiepusha na janga hilo.

0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia