Ticker

6/recent/ticker-posts

JAMBAZI SUGU LAUWAWA

Jambazi sugu mkoani Arusha,Manyara na Kilimanjaro Ismail Nicolaus {46} maarufu kwa jina la ‘’Tumbonii’’ limeuawa kwa kupigwa risasi na mtu anayedaiwa kuwa ni jambazi mwenzake wakituhumiana kurushana fedha za wizi.

Tukio la kuuawa kwa jambazi hilo na  mwenzake limetokea eneo la Bomangómbe mkoani Kilimanjaro juni 22 mwaka huu na mwili wake kutelekezwa katika hospital ya Mawenzi mkoni humo.

Habari za uhakika ambazo libeneke la kaskazini inazo zilisema kuwa Tumbonii aliuawa na jambazi mwenzake  kwa kupigwa risasi na kufa hapo hapo katika tukio lililotokea  eneo hilo.

Vyanzo vya habari viliendelea kusema kuwa kupigwa risasi kwa tumbonii na huyo jambazi mwenzake ni kufuatia kutapeliana mamilioni ya fedha walizoiba wiki moja kabla ya kifo chake.

Habari zilisema kuwa jambazi aliyempiga risasi Tumbonii ndiye aliyekimbia na mamilioni hayo ya fedha.

‘’Wale majambazi walitapeliana na  marehemu alitangaza kumuua pindi watakapokutana lakini amekufa yeye baada ya mwenzake kumwai''alisema mtoa habari

Habari zilisema marehemu Tumboni aliokotwa na kupelekwa katika chumba cha maiti cha hospital ya mkoa ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro .

Vyanzo hivyo vilisema ndugu marehemu alipopata taarifa za nduguye kuuawa alikwenda polisi Arusha ili kupata taarifa lakini alidai kuwa hakupata ushirikiano juu ya hilo lakini polisi wema walimwambia kuwa nduguye yuko chumba cha maiti Moshi na ameuawa.

Habari zilisema alikwenda Hospital ya Mawenzi juni 26 mwaka huu na kuuchukua mwili huo na kesho {leo} Jambazi Tumbonii anazikwa nyumbani kwake Kimandolu Jijini Arusha.


Kamanda wa polisi Mkoani Arusha Liberatus Sabas alipoulizwa juu ya kifo cha jambazi huyo alisema kuwa hana taarifa juu ya hilo lakini alikiri kuwa jambazi huyo alikuwa akitafutwa sana na jeshi hilo kwa muda mrefu bila ya mafanikio kutokana kutokana na kuhusika na uhalifu mkoani

Jambazi hilo linasifika kwa matukio makubwa ya uporaji na maisha yake yote amekuwa akitumikia gerezani hali iliyompa umaarufu mkubwa
habari imeandikwa na mdau wa libeneke la kaskazini  Joseph Ngilisho

Post a Comment

0 Comments