Rais wa Gambia, Fatou Bensouda ameapishwa kuwa Mwendesha Mashitaka mpya wa Mahakama ya Kimataifa
ya Makosa ya Jinai (ICC) iliyopo The Hugue, Uholanzi, kuchukua nafasi
ya Luis Moreno Ocampo kutokaArgentina, ambaye mkataba wake wa kazi wa miaka tisa umemalizika.
Mwanasheria huyo mwenye umri was miaka 50 alikuwa naibu wa Ocampo
tangu mwaka 2004.Alichaguliwa kuwa Mwendesha Mashitaka wa ICC na
Mkutano Mkuu wa Nchi zilizotia saini mkataba wa Roma, kuanzisha ICC
(ASP), Desemba 12, 2011.
Katika sherehe hiyo fupi, Mwendesha Mashitaka huyo mpya, aliahidi
kutekeleza majukumu yake na kutumia madaraka yakekamaMwendesha Mashitaka
wa Mahakama hiyo’’kwa heshima, uaminifu, bila upendeleo na kwa
utashi,’’
Sherehe hiyo iliongozwa na Rais wa ICC, Sang-Hyun Song, ambaye
alielezea matumaini yake kwamba ‘’sauti yake huru na yenye
nguvu,utaalamu wa sheria na kujihusisha kwake vilivyo na masuala ya haki
za binadamu vitachangia kwa kiasi kikubwa katika mapambano ya vita
dhidi ya uhalifu.’’
Waliohudhuria sherehe hizo ni pamoja na majaji wa mahakama hiyo,
maafisa wa idara ya usajili, mwendesha mashitaka analiyemaliza muda
wake,Moreno-Ocampo na watu wengine mashuri kadhaa akiwenmo Rais wa ASP,
Tiina Intelmann, ambaye ndiye aliyemwapisha mwendesha mashitaka huyo
mpya.
Bensouda hapa awali alikuwa
akifanyakazikamaMshauri wa sheria katika Mahakama ya Kimataiafa ya
Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) kabla ya kujiunga na ICC.