makabidhiano ya komputer
Shirika lisilo la kiserikali la Hope For Tanzania limetoa computer 92 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15 kama mchango wa kuinua kiwango cha elimu katika shule nne jijini Arusha.
Shirika lisilo la kiserikali la Hope For Tanzania limetoa computer 92 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15 kama mchango wa kuinua kiwango cha elimu katika shule nne jijini Arusha.
Wakurugenzi wa
shirika hilo hapa Tanzania Felex Masenge na Naomi Masenge wamesema kuwa msaada huo
unatokana na wafadhili wa shule isiyo ya kiserikali ya Tuishime ambao waliahidi
kuzisaidia shule 10 jijini arusha vifaa hivyo
ili wanafunzi waweze kujifunza somo la Tehama.
Felex amesema
kuwa zoezi hilo la kupatiwa computer linaendelea hali ambayo itatoa fursa kwa shule
hizo kufanya vizuri kielimu katika ulimwengu wa sasa wa sayansi na teknolojia.
Akikabidhi computer
hizo kwa wakuu wa shule hizo ambazo ni
shule ya msingi uhuru,ukombozi,kijenge na tuishime mgeni rasmi katika
hafla hiyo Afisa elimu vielelezo Godfrey Augustino amesema kuwa vifaa
hivyo vimekuja wakati muafaka na amewataka kuvilinda na kuvitunza vizuri.
Pia amesema kuwa
shule nyingi za serikali zinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa fedha hali ambayo inapelekea kushindwa kununua computer na wanafunzi kushindwa kufanya mitihani ya
Tehama kama ilivyo kwa shule zinazomilikiwa na watu binafsi.
Aidha Augustino
ametoa wito kwa wakuu hao wa shule kuzitunza na kuzilinda na kuwa hatokuwa tayari kupokea taarifa
ya kupotea ama kuibiwa kwa vifaa hivyo bali
hatua kali za kisheria zitachuliwa dhidi ya mwalimu husika.
Lakini hata hivyo
amewataka walimu kwenda shule na kwenda kujifunza alimu ya computer ili waweze
kuwafundisha wanafunzi somo hilo la Tehama na hatimaye waweze kufanya vizuri
katika mitihani yao.
Akiongea kwa niaba
ya wakuu wa shule diwani wa kata ya sokon one Michael Kivuyo amesema kuwa ni
vyema watanzania wakaiga mfano huo kwa kuchangia kuinua elimu katika shule za msingi
na sio kuchangia ama kutoa msaada kwa mambo yasiyo ya msingi katika jamii.