KESI YA SABA TOKA ICTR YAKUBALIWA KUHAMISHIWA RWANDA
Mahakama
ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Jumatatu ilikubali
maombi ya mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo kuhamishia nchini Rwanda
kesi ya mshitakiwa, Aloys Ndimbati.
Hii ni kesi ya saba toka ICTR kupelekwa kusikilizwa katika mahakama za Rwanda.
Katika
uamuzi wake, Mahakama iliyokuwa inaongozwa an Jaji Vagn Joensen
imemwamuru mwendesha mashitaka wa ICTR kumkabidhi Mwendesha Mashitaka
Mkuu wa Rwanda, nyaraka zote zinazounga mkono mashitaka dhidi ya
mtuhumiwa ambaye bado anasakwa na mahakama hiyo, mapema iwazekanavyo.
Amri hiyo inatakiwa kutekelezwa katika kipindi cha siku 30 tangu kutolewa kwa amri ya mwisho ya kuhamishwa kwa kesi hiyo.
Mahakama
ilielezea matumaini yake kwamba ‘’Jamhuri ya Rwanda, kwa kubali kesi
toka ICTR, itatekeleza kwa vitendo ahadi iliyotoa juu ya kuzishughulikia
kesi hizo kwa nia njema, uwezo ulio nao na utayari wa kuzingatia
viwango vya juu vya kimataiafa vya utendaji haki.’’
Ndimbati,
Meya wa zamani wa wilaya ya Gisovu, mkoa wa Kibuye, Magharibi ya
Rwanda, anashitakiwa kwa mauaji ya kimbari, kula njama za kufanaya
mauaji hayo, uchochezi na uhalifu dhidi ya binadamu kwa kuua, kuteketeza
kizazi, ubakaji na utesaji.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia