Ticker

6/recent/ticker-posts

DIWANI ACHANGIA UJENZI WA ZAHANATI

JUMLA ya  shilingi  Milioni 160 zimechangwa  katika harambee ya kuchangia  ujenzi wa hosptali  maalumu kwa ajili ya kina mama na watoto katika kata ya Sombetini jijini arusha .

Harambee hiyo iliongozwa na Diwani wa kata ya Mlangariini
Mathias Manga ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu wa madini jijini Arusha ,ambapo alitoa kiasi cha shilingi milioni 20 na kufuatiwa na watu mbalimbali walioalikwa.
Manga alisema kuwa ujenzi wa hospitali  hiyo utasaidia kupunguza kero kwa akina mama ya kufuata huduma ya matibabu umbali mrefu iliyokuwa ikisababisha  wengi wao kujifungulia njiani .
Alisema lengo la harambee hiyo ni kupatikana kwa kiasi cha shilingi milioni 200 ambazo zingewezesha kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo inayomikiliwa na kanisa  katoliki Parokia ya moyo mtakatifu wa Yesu kata ya Sombetini  .

Aidha diwani Manga alisema  kuwa ameamua kushiriki katika harambee hiyo kwa kuwa anajua kuwa wajibu wa kiongozi yoyote yule  ni kushiriki huduma za kijamii pasipo kuzikwepa au hata kutoa ahadi ambazo hazitekekelezeki katika jamii.

“ndugu zangu sisi wanasiasa tumekuwa tukisifika sana kutoa ahadi ambazo hazitekelezeki ila kwa upande wangu napenda niwahakikishie yakuwa kiongozi si kuahidi tu bali ni kutekeleza na jamii inafarijika kuona kiongozi anakuwa mstari wa mbele kuhudumia jamii’’alisema Manga

Diwani huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo alisema kuwa  kiongozi anatakiwa kuhakisha harakati zote za kuiletea jamii maendeleo zinapiga hatua hususani kwa mambo muhimu kama ujenzi wa shule ,  Hosptali ,barabara pamoja na Uboreshaji wa Miundo mbinu.

Kwa upande wake Padri wa parokia  hiyo Padri Moses Mwaniki Gitau amewaondoa shaka wakazi waishio katika kata ya Sombetini  jjini  Arusha kwa ujumla kuwa hospitali hiyo ikikamilika itakuwa mkombozi kwo kwa kuhudumia wakazi wote bila ya kujali itakadi za kidini ama kisiasa na wale wasiojiweza watapewa kipaumbe cha kupata matibabu.

Wakati huo huo mwenyekiti wa harambee hiyo Joseph Masawe  alisema imefika muda muafaka kwa watanzania kujitolea kwa hali na mali katika kujenga mahitaji muhimu yaliyopo ndani ya jamii ikiwemo shule, Vituo vya
afya na sio kutegemea wafadhili kutoka nje.

Hata hivyo ametoa wito kwa jamii nchini kubadika kimtazamo kuchangia miradi yenye tija ya maendeleo kwa jamii sio kuchangia vitu vye manufaa kwa watu wachache kama sherehe sambamba na mambo ya anasa ambayo hayana faida kwa jamii.

Post a Comment

0 Comments