mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Edward hosea akiongea na waandishi wa habari
Dola za Kimarekani Bilion 148huwa zinapotea ndani ya Nchi za bara la Afrika kila mwaka kutokana na kuwepo kwa mianya mingi ya rushwa na badala yake fedha hizo zinapelekwa katika nchi za Ugaibuni hali ambayo inasababisha madhara makubwa sana kwa wananchi wan chi hizo.Hayo yameelezwa na mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)Dkt Edward hosea wakati akizungumza katika mkutano wa bodi ya ushauri wa masuala ya Rushwa kwa nchi za bara la Afrika mapema leo jijini hapa
Aidha dkt Hosea alisema kuwa kiwango hicho cha fedha hupotea kutokana na baadhi ya mianya ya Rushwa ambayo imo kwenye nchi hizo na badala yake fedha hizo zinapelekwa kwenye nchi za Ugaibuni
Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo ya upotevu wa fedha hizo unachangia kwa kiwango kikubwa sana hata kukithiri kwa rushwa ndani ya Nchi hizo hali ambayo nayo inachangia hata maendeleo duni ya nchi hizo za bara la Afrika
Katika hatua nyingine alisema kuwa mpaka sasa kwa Upande wa Serikali ya Tanzania tayari imeshaanza miachakato mbalimbali ya kujenga bodi ya kupambana na Rushwa ambapo mchakato huo pia utasaidia sana kupunguza wimbi kubwa sana la Rushwa hapa nchini.
Dkt Hosea alisisitiza kuwa ujenzi wa jengo la bodi hiyo ya kupambana na rushwa utaaanza mara baada ya Kupitishwa kwa bajeti yake ambapo jengo hilo litajengwa ndani ya eneo la Kisongo mkoani Arusha