RAIS AMUNGA MKONO OMBI LA SEREKALI YA IVORY COASTE


 Waandishi wakielekea katika uwanja wa ndege kia


RAIS Jakaya kikwete, ameunga mkono  ombi la serikali ya IvoryCoaste,au  Coute D"voure,, ya kutaka kurejeshwa makao makuu ya benki ya maendeleo ya Afrika, AFBD nchini humo kutokana na kumalizika kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe  ambayo ilisababisha makao makuu ya benki hiyo kuhamishiwa nchini Tunisia.

Rais, alitoa kauli hiyo  katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro mara baada ya kumuaga rais Allassane ouattara wa Senegar, aliyekuwa mjini arusha akihudhuria mkutano mkuu wa magavana wa benki ya maendeleo barani Afrika,

Akijibu maswali ya waandishi habari rais kikwete, amesema kuwa makao makuu ya benki hiyo yalihamishwa nchini  Coute D"oure, kutokana na machafuko yaliyotokea nchini humo lakini tayari amani imesharejea nchini  vivyo hakuna sababu ya makao makuu ya benki hiyo kuendelea kuwepo nchini Tunisia .

Rais kikwe tepia ameishukuru benki hiyo kwa kuleta mkutano huo mkubwa hapa nchini ambao unafanyika kwa mara ya kwanza tangia benki hiyo ianzishwe miaka 47 iliyopita na kusema kuwa hiyo ni heshima kwa Tanzania na kusema hiyo ni heshima ya kipee na ya juu kwa nchi yetu tulipewa na benki hiyo.

Akizungumza,kwa lugha ya Kifaransa, katika mkutano wa ufunguzi ,rais wa Allassane outtara,aliiomba wajumbe wa mkutano huo kukubali kurejeshwa makao makuu ya benki hiyo nchini kwake kwa kuwa amani imesharejea na hivyo kazi zitafanyika kwa ufanisi .

Outtara, amesema hakuna haja ya makao makuu ya benki hiyo kuendelea kubakia nchini tunisia ,hivyo akawaomba waangalie uwezekano wa kurejesha makao makuu nchini mwake .

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia