SEREKALI KUANZISHA BENKI YA WAKULIMA
Naibu waziri wa fedha, Mbene akiwa na Mwenyekiti wa AADFI na Mkurugenzi mtendaji wa TIB, Peter Noni.
SERIKALI inaanzisha benki ya wakulima nchini ambayo
itakuwa ikitoa mikopo mikubwa na ya muda mrefu ili kuboresha sekta ya kilimo
nchini ambayo ndiyo tegemeo kubwa katika kutoa ajira na kuongeza kipato cha
wananchi wengi.
Aidha imekubali kuongeza mtaji kwenye benki ya rasilimali
nchini (TIB) ili kuiwezesha kuwa na uwezo wa kutoa fedha zitakazotumika kwenye
miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini ikiwemo ile ya uboreshaji wa miundo
mbinu.
Hayo yalisemwa na Naibu waziri wa fedha, Janeth
Mbene mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa 38 wa Taasisi za Benki za Maendeleo
barani Afrika (AADFI) unaofanyika kwenye hoteli ya Arusha palasi ambapo
mwenyekiti wake ni Mkurugenzi mtendaji wa TIB, Peter Noni.
Alisema kuwa serikali imekubali kutenga kati ya dola za
Marekani milioni 400 na 500 kwa ajili hiyo ambapo benki hiyo ya wakulima inatarajiwa
kukamilika wakati wowote ndani ya mwaka huu kwani mchakato wake ulishaanza.
Awali akimkaribisha Naibu Waziri, Mbene kufungua mkutano
huo Mwenyekiti wa AADFI, Noni alisema kuwa ujenzi wa majengo kwa makao makuu ya
taasisi hiyo zilizoko Abidjan, Ivory Cost unaoendelea vizuri na kuwataka
wanachama wa taasisi hiyo kuendelea kuchangia kama walivyokubaliana.
Akiongea
kabla ya kufunguliwa warsha yao ya siku moja iliyofanyika may 29 na 30 mwaka huu ,
Noni ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji
wa TIB alizitaka nchi za Afrika kuziongezea mitaji benki hizo za Maendeleo ili kuzijengea
uwezo wa kuwasiliana na taasisi za fedha ndanui na nje ya nchi hivyo kuwa na
fedha za kutosha kutumika kwenye uboreshaji wa miundombinu ya barabara ambayo
ni nguzo muhimu ya maendeleo.
Alisema
kuwa suala la uboreshaji wa miundombinu kwenye nchi
za Afrika ikiwemo Tanzania linahitaji kiasi kikubwa cha fedha hivyo haliwezi
kufanikiwa endapo serikali zitaendelea kutegemea mikopo ya benki kubwa za
kimataifa na bajeti zao pekee badala yake zimeshauriwa
kushirikiana na benki za maendeleo zilizopo kwenye nchi zao.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia