MKUU WA WILAYA YA HAI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA POLISI WILAYANI HUMO AKUMBANA NA MATATIZO LUKUKI YANAYOKIKABILI KITUO HICHO

 mkuu huyo wa wilaya Novatus Makunga akiwasili akisindikizwa na mkuu wa polisi wilayani hao OCD Isaya Mbughi na maofisa wengine

Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Mhe.Novatus Makunga leo amefanya ziara katika makao makuu ya jeshi la polisi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro na kuongea na askari polisi wa wilaya hiyo

 askari wakiwa wanamsikiliza kwa makini mh.Novatus  Makunga Dc wa Hai

  maafande mbalimbali wakitoa maoni yao katika mkutano wao na mkuu huyo wa wilaya
Jeshi la Polisi wilayani Hai linakabiliw ana matatizo makubwa ya ukosefu wa  mafuta pamoja  na uboifu  wa magari  hali inayochangia jeshi hilo kushindwa kukabiliana na uhalifu uliokithiri wilayani humo

Hayo ameelezwa jana na askari polisi   wa wilaya hiyo  wakati wa mkutano wao  wa kwanza na mkuu wa wilaya hiyo  Novatus Mhando Makunga alipotembelea makao makuu ya polisi wilayani  humo


Miongoni mwa  chanagmoto hizo ni ukosefu wa nyumba za makazi ya askari, askari kutopandishwa vyeo kwa  miaka mingi pamoja na  askari kukosa vitendea kazi  yakiwemo makaratasi


Kutokana na  hali hii  Mkunga ameahidi kuzibeba na kuzifikisha ngazi ya juu ya jeshi hilo  pamoja na serikali ya mkoa


Askari hao  wamemweleza  Mkuu huyo wa wilaya kuwa  wamekuwa  wakitupiw alawama kutokana na kushindwa kufika maeneo ya matukio ya uhalifu kutokana na ubovu wa magari mawili yaliopo  katika kituo hicho pamoja na kukosa mafuta

Wametoa mfano kwamba pindi kunapoitokea taarifa za uhalifu mkuu wa  polisi  wilayani humo ama ofisa upelelezi   wanalazimika kutoa fedha zao mfukoni ili kununua mafuta ndipo askari  waweze kufika eneo la tukio


Hali hii haitendi haki kwa  askari  hao kununua mafuta wakati wakitumikia taifa huku seriali ikiwa kimya katika kutatua matatizo  hayo ya kushindw akutoa fedha za uendeshaji   pamoja na magari ya uhakika ili kukabiliana na uhalifu

Wamesema  wilaya ya hai inakabiliwa na uhalifu mwingi  ukiwemo wa biashara ya gongo, ujambazi pamoja na migogoro kati ya wafugaji na wakulima


Aidha askari hao pia wamemweleza mkuu wa wilaya  makunga kwamba kuekuwepo na ufinyu wa ofisi  ambapo mfano  askari wa kikosi  cha usalama barabarani wapatao 30 hutumia ofisi mmoja yenye ukubwa wa mita za mraba  saba kwa kumi


Pia kituo hicho cha polisi hakina samani mfano askari polisi  hukaa kwenya mawe wakati wakishughulikia masuala mbalimbali ya kesi


Baadhi ya askari  wamemweleza mkuu  huyo wa wilaya kuwa  jeshi la polisi wilayani humo linaweza kuingia katika madhara na vishawishi vingi vibaya kutokana na kutegemea misaada ya mafuta kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa wilayani humo  vishawishi ambavyo ni hatari kwa utendaji wao  wa kazi za kiaskari


Baadhi yao wamesema wamekuwa katika jeshi hlo kwa zaidi yamiaka 20  bila kuajiriwa na badala yake  wamekuwa vibarua miaka yao yote hasa askari wa ngazi ya chini


Kuhusu suala la likizo mkuu wa polisi wilayani humo SP Isaya Mbughi amemweleza mkuu wa wilaya makunga kwmaba  askari wengi  wilayani huo wanashindwa kwenda likizo kutokana na baadhi yao kuuza likizo zao na kushindwa kwenda maeneo  walikozaliwa badala yake wamekuwa wakililaumu jeshi la polisi


OCD Mbughi alisema  lipo tatizo kubwa la biashara ya gongo linalochangiwa na baadhi ya viongozi wa vijiji wanaoshiriki katika biashara hiyo wilayani humo

Akizungumza na askari polisi hao Mkuu wa wilaya Makunga  aliwataka waimarishe mshikamano katika kukabiliana na uhalifu  liiwemo tatizo la gongo


Mkunga alisisitiza kuwa askari polisi  ni lazima wawe kitu kimoja ili  kuweza kudhibiti uhaliufu wilaya ni humo


Kuhusu mjadala wa mabadiliko ya katiba, Makunga aliwataka askari polisi hao kushiriki kikamilifu kutoa  changamoto zitakazosaidia  kasoro zilizopo katika uendeshaji wa jeshi hilo zinazopaswa kuingizwa Katika katiba hiyo


Amesema katiba ndiyo nguzo kuu  ya kuongoza masuala mbalimbali ya nchi hivyo ni wajibu wa askari polisi kuhakikisha masuala yao yote muhimu yanaingizwa katika katiba hiyo

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia