MDAHALO
Wafanyakazi wa radio sunrise wakiongozwa na severinus mwijage wakifatilia kwa makini mdahalo ulikuwa umeandaliwa na ANGONET uliokuwa unafanyika katika hotel ya Golden rose jijini hapa
mtoa mada ambaye ni mkuu wa wilaya ya mbeya Noman Sigalla
HALMASHAURI mbalimbali ndani ya Nchi ya Tanzania zimetakiwa kyuhakikisha
kuwa zinakuwa wazi hasa wakati watakapokuwa wanapanga bajeti ili kuziepusha na
matatizo mbalimbali
Hayo yameelezwa na
mwanaharakati wa mambo mbalimbali hapa nchi BwMarcos Albwane wakati
akizungumza katika mdahalo kuhusu uwazi na uwajibikaji katika kusimamia rasilimali za nchi
Alisema kuwa uwazi ni kipengele muhimu sana
na kwa hali hiyo ni vema hata halmshauri nazo zikatekeleza mpango huo tofauti
na sasa ambapo kuna changamoto lukuki sana
Aliongeza kuwa endapo kama hali hiyo itafanikishwa ndani ya
halmashauri hasa wakati wa upangaji wa bajeti basi hali hiyo itachangia kwa
kiwango kikubwa sana hata kwa watendaji wa halmashauri kuwa na dhana ya
uwajibikaji wa hali ya juu sana
Alisema kuwa dhana hiyo pia inaenda sanjari na dhana ya
uwajibikaji kwa viongozi wa
halmashauri kwa kuwa utaweza hata
kuboresha utendaji wa Serikali kuu na serikali za mitaa hivyo kuendeleza kukua
na kuimarisha utawala bora
Alifafanua kuwa katika Serikali za mitaa ni muhimu sana kuwezesha ushiriki wa
wananchi katika mchakato mzima wa kuweza kufanya maamuzi ambapo kwa sasa tayari
Serikali imeshaweza kuongeza idadi ya uwajibikaji
Hataivyo mdahalo huo uliwashirikisha wadau zaidi ya 500 kutoka
katika maeneo mbalimbali ya Arusha huku lengo likiwa ni kujadili juu ya
rasilimali za taifa ambazo wananchi wanatakiwa kuzitambua


0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia