MATUKIO ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi
ya wanawake yamezidi kushamili miongoni
mwa jamii na makabila tofauti hapa nchini.
Msichana mwenye umri wa miaka 20,Neema Palangyo mkazi
wa Sanawari ya juu jijini Arusha, hata sahau mateso na manyanyaso anayoyapata
kutokana na ukatili wa kutisha
anaofanyiwa na mumewe katika kipindi chote
cha maisha yao tangu aolewe mwaka 2011.
Neema akiwa na mtoto wake mchanga mgongoni, anaeleza
kwa uchungu huku akibubujikwa na machozi
na kusema kuwa kila akilitaja
jina la mumewe aitwaye Evance Mushi(28)alimaarufu Mjasiriamali ,machozi
humtoka kwani anakumbuka unyama anaofanyiwa , ambapo pamoja na kipigo cha mara
kwa mara anachokipata kutoka kwa mumewe huyo analalamikia udhalilishaji wa
kutumiwa kinyume cha maumbile bila ridhaa yake.
Anasema pamoja na ukatili huo amekuwa akitaka kumuua
mtoto wao mdogo mwenye umri wa miezi mine,kwa lengo la kumtoa sadaka kwa mganga
wa kienyeji aliyeko eneo la Njiro jijini
Arusha ambaye anatoa huduma ya freemason itakayomfanya awe tajiri wa maisha
bora.
Kwa mujibu wa Neema anasema hakuwahi kuyafurahia
maisha ya kuolewa hata siku moja kwani licha ya kumtimizia kila kitu ,amedai
kuwa mumewe huyo amekuwa katiri ,haridhiki na huduma za kimahusiano anazompatia
na amekuwa akimlazimisha kumwingilia kinyume na maumbile mara kwa mara na kumfanya aharibike vibaya
sehemu zake.
Aidha amedai kuwa mtoto wake mdogo ndio anayefanywa
fimbo ya kupigiwa ambapo amekuwa akinyangánya mgongoni na kuanza kumpiga nae
akidai anataka amuue yeye na mtoto wake akatoe
sadaka damu yao ili aondokane na umaskini alionao.
Neema ambaye ni mzaliwa wa Songoro wilayani Arumeru,anasimulia kuwa aliolewa na Mjasiriamali mwaka 2011
akiwa na umri wa miaka 19 ,ambapo maisha
yao yalikuwa ni kupigwa mara kwa mara na kipigo hicho kilitokana nay eye
kukataa kutumiwa kinyume na maumbile.
Alisema msimamo wake wa kutotaka kutumiwa kinyume na
maumbile kulisababisha anyimwe matumizi ya ndani na kujikuta akishinda na njaa
huku mumewe huyo mara nyingine akimkejei kuwa siku akikubali kufanya mapenzi
kinyume na maumbile angemlipa ujira wa shilingi 5000.
Anaeleza kuwa siku moja mumewe alirudi nyumbani usiku
akiwa amelewa na alipomfungulia mlango
aliingia ndani na kuanza kumpiga sana huku akimvua nguo zote na kuanza kumbaka
kwa kumwingilia kinyume na maumbile ,wakati huo alikuwa na ujauzito wa miezi
nane.
Anadai kipigo kiliongezeka zaidi alipomfahamisha kuwa
alikuwa na ujauzito wa miezi nane ambapo
mwanaume huyo alimwambia hakuwa tayari kulea mimba hiyo na alikuwa akimpiga
tumboni na vitu vizito na kumbaniza ukutani, anasema alilia sana kwani katika
maisha yake hakuwahi kupata mateso ya aina hiyo.
''kesho yake niliamua kuondoka nyumbani hapo na kwenda
kwa kaka yangu aitwaye Emanuel Palangyo kwa lengo la kupata msaada ''anasema
Aliongeza akiwa nyumbani kwa kaka yake msaada uligeuka
shubiri kwani kaka yake alimfanyia unyama mwingine wa kutisha kwani akiwa
amelala usiku alimbaka na kufanya naye mapenzi huku akimtishia kumuua akidai
kuwa atakuwa atapata utajiri baada ya tukio hilo.
''nilivumilia mateso hayo ya kubakwa kila mara na kaka
yangu kwani sikuwa na msaada mwingine maana hali yangu ilikuwa mbaya sana na
tumbo langu liliongezeka ukubwa nikawa sijiwezi,kaka aliendelea kunibaka bila
kujali mimba niliyonayo tena bila hata kutumia mpira(condom)''alisema Neema.
Siku moja wakati kaka yake ameenda kwenye shughuli
zake alifungasha viti vyake na kuamua kurudi kwa mumewe akiamini labda atakuwa
amebadilika tabia ,hata hivyo mambao
yakawa tofauti na matazamio yake.
Anasema siku aliyofika mumewe hakuwepo majira ya usiku
alirudi na kumkuta ambapo alianza kumpiga na kumvua nguo zote na baadae
alimbaka kinyume na maumbile .
Ilipofika mwezi wa pili mwaka huu alijifungua salama
katika hospitali ya mkoa Mount Meru mtoto wa kike kwa msaada wa wasamalia wema ,wakati huo
alikuwa akifanya kazi ya kufua na kuosha vyombo kwa watu ili apate fedha za
kumnunulia maziwa mtoto wake.
Anaongeza kuwa mumewe huyo aliendelea kumbaka bila
kujali ametoka kujifungua na kisha kumtelekeza nyumbani bila kumwachia fedha ya
matumizi,hata hivyo anadai kuwa mumewe amekuwa akimnyoa nywele za mtoto huyo na
kumkata kitovu na kupeleke viungo hivyo kwa mganga wa kienyeji.
Kwa sasa msichana huyo anaishi maisha ya taabu na
anaomba msaada kwa wasamalia wema,mashirika na watetezi wa haki za binadamu
wamsaidie aweze kumudu maisha ya kumtunza mtoto wake na kupata fedha za kula
,ambapo katikati ya mwezi huu ameamua kuhama kwa mwanaume huyo akiogopa kuuawa.