WIZARA ya Nishati na Madini hususan Ofisi ya madini kanda ya kaskazini wamekea vikali wachimbaji wa madini ambao wamekuwa wakitumia baruti kama silaha mbadala ya kuzitumia kama nyenzo za kazi ya uchimbaji.
Akizungumza
na wandishi wa habari kamishna wa madini kanda ya kaskazini Mhandisi
Benjamini Mchwampaka amesema kuwa vitendo hivyo viovu vinatokana na
wachimbaji wa wasiokuwa na maadili ya uchimbaji madini ambao wanatumia
baruti kutengeneza mabomu ya kienyeji na kuwatupia wachimbaji wa migodi
ya jirani.
Mhandishi
Mchwampaka ameongeza kuwa ofisi yake haitolifumbia macho suala hilo kwa
kuwa huo sio uchimbaji bali ni uhalifu kwa kuwa una lengo la kuwaumiza
na kuwatisha kusudi wawafukuze ili kuchukua maeneo yao ambayo yanahisiwa
kuwa na uzalishaji wa madini.
Aidha ametaja maeneo ambayo vitendo hivyo vimeshamiri sana kwenye migodi inayopakana na moigodi ya Kampuni ya Tanzanite One kwenye kitalu C.
Amefafanua
kuwa mgodi wowote ambao utabainika kwamba wachimbaji wake wanajihusisha
na vitendo vya kuwatupia mabomu wachimbaji wa migodi jirani,mgodi huo
utafungwa mara moja na leseni husika itafutwa na wahusika wote
watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Pia amewataka Mameneja na wachimbaji kuwa ni lazima kutangaziana baruti ama moto kabla ya ulipuaji baruti kufanyika ili kuthibiti vitendo viovu.