Mahakama Maalum ya Sierra Leone (SCS) Jumatano wiki hii imemhukumu
kifungo cha miaka 50 jela Rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor
baada ya kumtia hatiani kwa mashitaka 11 yaliyokuwa yanamkabili ikiwa ni
pamoja na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.
Majaji wa mahakama hiyo walikataa maombi yote ya kumpunguzia
adhabuTaylor. Jaji Kiongozi wa katika kesi hiyo, Richard Lussick alisema
kwamba ‘’ uongozi hauna budi kuendeshwa kwa kushughulikia uhalifu na
siyo kwa kufanya uhalifu.’’
Muda mfupi baada ya hukumu hiyo kutolewa Wakili waTayloralitangaza
kwamba atakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo. Iwapo hukumu hiyo
itadhibitishwa, adhabu hiyo ni sawa na kifungo cha maisha kwa Rais huyo
wa zamani mwenye umri wa miaka 64.
Mahakama katika kumtia hatiani
ilieleza kuwaTayloralilipatia kundi la waasi la RUF nchiniSierra
Leonemisaada ya kijeshi, kioperesheni na fedha huku akijua kwamba
walikuwa wanatenda uhalifu mkubwa ikiwa ni pamoja na mauaji,
ubakaji,utumwa wa ngono,kuwasajili na kuwatumia watoto chini ya miaka 15
katika mapambano.
Mwendesha mashitaka alipendekeza adhabu ya kifungo cha miaka 80 jela.
Hukumu hiyo ilikuwa inatolewa toka mjini The Hague, Uholanzi na kurushwa moja kwa moja kwa mtandao wa intaneti.
Kesi yake ilianza kusikilizwa Juni 2007. Mwendesha mashitaka iliita
mashahidi 94 wakiwemo 32 ambao walikuwa ni marafiki wa karibu
waTaylorambao hatimaye walitoa ushahidi dhidi yake.
Tayloraliandaliwa mashitaka Juni 2003 lakini hati ya kukamatwa kwake
ilibakia kuwa siri hadi alipokubali kuachia madaraka Agosti 2003, bada
ya kupewa hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa nchiniNigeria.
Machi 2006,
alitiwa mbaroni nchiniNigeriana kisha kusafirishwa hadi katika mahakama
ya SCSL.
Serikali ya Uholanzi ilikubali kupokea kesi hiyo kusikiliziwa nchini
mwake kufuatia ombi la Rais waLiberia, Ellen Johnson Sirleaf, ambaye
alikuwa anahofia kuzuka kwa ghasia iwapo kesi hiyo ingesikilizwaSierra
Leone.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia