MKUTANO WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA NI CHANGAMOTO KUBWA KWA NCHI YETU

 
 
Mkutano wa benki ya maendeleo y Afrika, AFDB, ni changamoto kwa benki zetu hapa nchini katika swala zima la kuchangia kukua kwa uchumi na benki zenywe kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko zilivyo sasa ili ziweze kwendana na mabadiliko ya kiteknolojia inayotokea ulimwenguni na kuweza kuepuka kupata hasara kunapotokea mitikisiko ya kiuchumi

Hayo yameelezwa na Askofu josephat mwingira, alipokuwa akizungumza na Libeneke la kaskazini h jijini hapa, anakohudhuria mkutano mkuu wa benki ya maendeleo ya Afrika ,na kusema  kuwa kutokana na mkutano huo tunahitaji kufikiria  upya juu ya mipango yetu kwa kushirikisha wadau wengi zaidi kuliko hali ilivyo sasa ili tuweze kupata maendeleo ya haraka  na hivyo kushindana na mataifa yaliyoendelea.


Alisema Afrika sio masikini ila inakosa uongozi imara wenye dhamira nzuri ya kuwafungua macho wananchi waweze kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kweli ya kiuchumi na kupata maendeleo endelevu .

''unajua nchi yetu sio masikini ila tatizo ni kwamba inakosa viongozi wenye uwezo na ambao wanauchungu na nchi yao ,mbali na hao pia wanauchungu na wananchi wao''alisema Mwingira

Alibainisha kuwa amesikitishwa na idadi ndogo ya washiriki kutoka sekta binafsi nchini huku, washiriki wengi  ni watumishi wa serikali na kutahadharisha  kuwa iwapo hali hiyo haitarekebishwa siku zijazo taifa halitaweza kusonga mbele katika mabadiliko yanayotarajiwa kwa sababu wadau ndio walengwa ila hawapewi nafasi ya kutosheleza kushiriki na kutoa mchango wao .

kuhusu,uwekezaji ,,askofu Mwingira, amesema bado ni tatizo kutokana na jamii haijaelimishwa vya kutosha hivyo kushindwa kushiriki kikamilifu na kwa wingi katika shughuli zote ili iweze kuleta mabadiliko katika maisha yao na hatimae kuondokana na umaskini kwa kuanzisha miradi ya kiuchumi na kuiendeleza.

Kwa upande wa wananchi walifurahi  na kusema kuwa mkutano huu umewaongezea kipato kwa kipindi kichache kwani wamekuwa wanafanya biashara sana na wamepata faida kubwa kutokana na wageni huku wakihisihi serekali kuendela kuleta mikutano mikubwa kama hii jijini hapa kwa inawasaidia wananchi na kuongezea kipato jiji letu

''kwakweli nimefurahia mkutano huu kwani umetusaidia kuchangamsha mji na kutupa fedha nyingi watu wamekuwa wakiuza vitu mbalimbali kwa ajili ya mkutano huu ivyo tunaomba serekali isitutupe bali ilete mikutano hii ili pato la jiji letu liendelee kukuwa"alisema  israel mungure.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia