WAKAGUZI WA HESABU ZA SEREKALI WAPIGWA MSASA
Wakaguzi wa mahesabu ya Serikali nchini
wametakiwa kufanya kazi hiyo kwa umakini kwa kufuata madili na taratibu
za kazi ya ukaguzi ikiwa ni pamoja na kutowaonea au kufanya upendeleo kwa
wanaowakagua ili kusaidia kuonesha dhamani ya matumizi ya fedha za Sererikali
zinazotolewa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hayo yalibainishwa jana na
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Ruth Malisa wakati wa ufunguzi wa
mafunzo ya wiki 3 kwa wakaguzi wa mahesabu ya Serikali kanda ya kaskazini
kutoka mikoa ya Tanga,Kilimanjaro,Arusha na Manyara mafunzo ambayo yameandaliwa
na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
Alisema kuwa taarifa ya wakaguzi inategemewa kwenye
shughuli mbalimbali za utafiti pamoja na wataalamu mbalimbali wa serikali
katika kuonesha dhamani ya fedha za Serikali,(value for money)hivyo hali hiyo
itasaidia wakaguzi kugundua na kuwa na taarifa nzuri za matumizi ya fedha za
serikali katika mambo mbalimbali.
“Wakaguzi wa mahesabu wanategemewa katika kutoa
maelekezo ya matumizi ya fedha za Seriakali kama jengo,au mradi wowote
uliotolewa fedha na Serikali kama kilichofanyika kimeendana na fedha
yenyewe,hivyo ni watu muhimu na wanapaswa kupewa mafunzo”Alisema Ruth.
Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa mafunzo kutoka
Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Felister Kenulembe alisema kuwa mafunzo hayo yamelengwa
kuwaongezea uwezo wakaguzi hususani ni kujifunza mifumo mipya ukaguzi.
Alisema kuwa wakaguzi wanatakiwa kuwa mbele katika
kuifahamu mifumo mipya ya ukaguzi ili wasichanganywe na wanaoenda kuwakagua
hali itakayosaidia kuandaa taarifa nzuri ambazo zinatonyesha matumizi mazuri ya
fedha za Serikali.
“Mifumo ya ukaguzi inabadilika mara kwa mara maana
tunatoa vipaumbele kwenye mafunzo ili wakaguzi waweze kuongeza ufanisi kwenye
ukaguzi,ambapo leo mafunzo haya pia tumefanyia kwenye jengo letu la wakaguzi
Mkoa wa Kilimanjaro ili kupunguza garama”Alisema Felister .
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia