KAMPENI YA ULINZI WA MTOTO HAI WAPUNGUZA ONGEZEKO LA WATOTO WA MITAANI
Kampeni
kubwa kwa jamii dhidi ya ulinzi wa mtoto
katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imewezesha kupungua kwa vituo vya
kulelea yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kutoka 22 hadi 7 na pia kuwarudisha
watoto 150 katika familia zao katia ya mwaka 2010 na 2012 wilayani humo.
Hayo
yameelezwa na Afisa wa maendeleo ya jamii katika halmashauri ya wilaya ya Hai Bi
Restina Mwasha wakati ujumbe wa maofisa wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa
watoto,UNICEF ulipokutana na mkuu wa wilaya hiyo Bw Novatus Makunga ofisini
kwake wilayani humo.
Bi
Mwasha ameeleza kuwa hivi sasa kiasi cha uelewa wa masuala yanayohusu ulinzi wa
mtoto katika wilaya ya Hai imefikia asiliamia 85 ingawa bado jamii pamoja na
mfumo uliopo hajaweza kuchululia kwa uzito unaotakiwa masuala ya mtoto.
Amefafanua
kuwa baadhi ya vituo vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira
magumu vimekuwa vikianzishwa zaidi kwa lengo la kuwanufaisha wamiliki wa vituo
hivyo kuliko kutatua matatizo ya watoto.
Ameeleza
kuwa mkakati huo ulichukuliwa kutokana na kushamiri kwa uanzishwaji wa vituo
vya watoto yatima kuanzia mwaka 2010 na hivyo nguvu zilielekezwa katika uelimishaji
wa jamii kuhusu suala zima la ulinzi wa mtoto.
Ameeleza
kuwa kampeni hiyo ililenga katika kupunguza idadi ya watoto wanaolelewa katika
vituo vya watoto yatima,kudhibiti vituo vinavyoendeshwa kwa kiwango cha chini
na kupunguza vitendo ukatili wa watoto.
Bi
Mwasha ameeleza kuwa zaidi ya masuala 587 yanayohusu ukatili wa watoto
yalishughulikiwa na baadhi kutatulia na mengine kupelekwa katika ngazi ya
kisheria kati ya mwezi Mei 2010 mpaka
machi 2012.
Ametaja
baadhi ya matukio kuwa ni pamoja na vipigo,ubakaji,usafirishaji kwa ajili ya
kufanyishwa kazi,wizi wa watoto,ujauzito,kuozwa,Lugha chafu na ajira mbaya.
Bi
Mwasha ameeleza kuwa wameweza kuendesha mafunzo kwa wadau mbalimbali ya ulinzi wa mtoto wakiwemo waalimu
342,wauguzi 40,polisi 76,maofisa magereza 2,wasikilizaji masahauri wa kata 14
katika
kuimarisha zaidi mkakati wa ulinzi kwa mtoto ameeleza kuwa mbali na timu ya
wilaya lakini pia tayari wameanzisha
timu za ulinzi katika ngazi ya kata kumi
na vijiji 55 huku kukibakiwa na uundwaji
wa timu nyingine katika kata mpya 4 na vijiji vipya 5
Hata
hivyo Bi Mwasha ameeleza kuwa bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu
wa ofisi ya kutosha kuweza kusikiliza
kwa faragha masuala ya watoto pamoja na ukosefu wa fedha za kutosha katika katika
bajeti
Aidha
Bi Mwasha amebainisha changamoto nyingine wanayokutana nayo ni dosari katika
fomu namba ya polisi inayotolewa kwa ajili ya matibabu kutokuwa na sehemu ya
jina kamili,cheo na taasisi ya daktari anayemuhudumia mtoto aliyeumizwa.
Hata
hivyo ameeleza kuwa baadhi ya watoto wamekuwa wakikumbana na mateso pamoja na
kwamba wanatoka katika familia zenye uwezo,masuala ya wataoto kudhulumiwa mali
na ndugu na baada ya kufariki kwa wazazi wao lazima iwe ajenda katika ulinzi wa
mtoto
Kwa
upande wake kiongozi wa ujumbe huo wa Unicef bi Mona Aika ameeleza kuwa wilaya ya Hai
imekuwa na mafanikio makubwa zaidi kutokana na utafiti uliendeshwa na mfuko huo
katika wilaya za Magu,Temeke na Hai kwa lengo la kuongezea nguvu mfumo wa mpangilio kwa ulinzi
wa mtoto nchini.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia