WAFANYAKAZI WA TANZANITE ONE KUBORESHEWA MASLAYI
UONGOZI wa Kampuni ya TanzaniteOne ya madini ya Tanzanite iliyopo
Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara imesaini mkataba wa kuboresha hali na maslahi
ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mkataba huo umefanyika baada ya
Majadiliano ya muda mrefu hatimaye menejimenti ya kampuni hiyo ikasaini mkataba
wa Kuboresha maslahi ya wafanyakazi kupitia Chama Cha Wafanyakazi wa Migodi (Tamico).
Katika kutia saini mkaataba huo juzi,kampuni
ya TanzaniteOne iliwakilishwa na Mkurugenzi wake Ndugu Wessel Morais na Ofisa rasilimali watu Johnson Mwani
na Tamico iliwakilishwa na Katibu mkuu Hassan Ameir,Katibu Tamico Kanda,Juma Bwikitia.
Kwa upande wa wafanyakazi wa
TanzaniteOne waliwakilishwa na Mwenyekiti wa Tamico wa Tawi hilo Raphael Alex
Ombade,Katibu wa Tawi,Richard Nyanginywa na wajumbe wote wa tawi la Tamico
Tanzanite One.
Akizungumza baada ya kutia saini kwenye
mkataba huo,Morais alisema kuwa ana heshimu
na kuthamini uwepo wa Chama Cha wafanyakazi migodini Tamico ambacho
kinatetea maslahi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
“Migongano na mitazamo tofauri ni
sehemu ya kazi na tatizo lolote litakalojitokeza liwasilishwe mezani na Tamico
kwa ajili ya majadiliano ya pamoja na kuweza kufikiwa muafaka wa pamoja,”
alisema Morais.
Katibu Mkuu wa Tamico Hassan Ameir
alisifu na kupongeza hatua iliyofikiwa na tawi kwa ushirikiano mkubwa wa TanzaniteOne
nakuthamini umuhimu wa kukaa meza moja kwa majadiliano kwani njia hiyo
hupunguza migogoro mingi.
“Viongozi wa wafanyakazi mzidishe
bidii,juhudi na maarifa katika uzalishaji ili kuongeza tija na ufanisi shemu
ya kazi na kupata nguvu ya kudai maslahi bora zaidi kwani huwezi kumkamua ng’ombe
maziwa bila kumlisha vizuri,” alisema Ameir.
Naye,Katibu wa Tamico Kanda ya
Kaskazini Juma Saidi Bwikitia alitoa shukrani zake za dhati kwa wote waliohusika
kwa namna moja au nyingine kuhakikisha kuwa mkataba huo unafanikiwa kutiwa
saini.
“Naziomba pande zote zilizosaini mkataba
kuuheshimu na kuutekeleza kwa vitendo kama taratibu za Kisheria zinavyosema na pande
wowote kutokwenda kinyume na yale waliyokubaliana ili kudumisha mahuisiano ya ajira
kwa mujibu wa Sheria,” alisema Bwitia.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia