OCAMPO ASHINIKIZA AL-BASHIR KUKAMATWA, KESI YA MUNYAGISHARI YAPELEKWA RWANDA
Mwendesha mashitaka wa Mahakama ya
Kimataifa ya Makosa ya Jinai, wiki hii alilihutubia Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa juu ya hali ilivyo nchini Sudan na kulitaka kutafuta
mbinu za kumkamata Rais Omar Al-Bashir na viongozi wengine nchini humo,
ilihali Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda iliamuru
kuhamishiwa nchini Rwanda kesi inayomkabili Bernard Munyagishari.
ICC
Ocampo ashinikiza kukamatwa kwa Al-Bashir: Mwendesha mashitaka wa
Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, Jumanne wiki hii alilitaka
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutafuta mbinu za kuwakamata
viongozi nchiniSudan, akiwemo Rais Omar Al-Bashir. Akilihutubia
Barazahilo, Ocampo alisisitiza kuwa kitendo cha serikali yaSudankukataa
kumkamata Al-Bashir kunatoa changamoto ya moja kwa moja juu ya mamlaka
lililonalo Barazahilo. Siku moja kabla ya kulihutubia Barazahilo,
mwendesha mashitaka huyo aliongea na mkosanyiko hukoNew York, ambapo
alipendekeza nchi zinazompokea Al-Bashir zinyimwe misaada,kamanjia
mojawapo ya kushinikiza kukamatwa kwake. Malawi Jumatatu ilitangaza
kumkamata Rais huyo waSudankamaatahudhuria kikao cha wakuu wa nchi
barani Afrika kitakachofanyika nchini humo mwezi ujao.
Mawakili wa Gbagbo waomba kusogezwa mbele kesi ya mteja wao: Mawakili
wa aliyekuwa Rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo Alhamisi wiki hii
waliiomba Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai kuahirisha hadi siku
nyingine kikao cha kuchambuakamamakosa yanayomkabili mteja wao
yanastahili kuthibitishwa. Awali, kikao hicho kilikuwa kimepangwa
kufanyika Juni 18. Mawakili hao walidai kuwa hali ya kiafya ya mteja wao
imemfanya ashindwe kutoa mchango mahususi katika maadalizi ya kikao
hicho. Mkuu huyo wa zamani wa nchi ambaye ni wa kwanza kushitakiwa
katika mahakama hiyo alifikishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Disemba 5,
mwaka jana ambapo alifahamishwa makosa yatakayomkabili ya uhalifu dhidi
ya binadamu yanayodaiwa kutendeka chini mwake kati ya Disemba 16, 2010
na Aprili 12, mwaka jana.
ICTR
Kesi ya Munyagishari yahamishiwaRwanda: Mahakama ya Kimataifa ya
Mauaji ya Kimbari ya Rwanda Jumatano ilikubaliana na maombi ya upande wa
mashitaka na kuamuru kesi ya mshitakiwa wa mauaji ya kimbari Bernard
Munyagishari ihamishiwe nchiniRwandakwa ajili ya kusikilizwa. Jopo la
majaji watatu walibainisha kuwa katika miaka ya hivi
karibuni,Rwandaimefanya mabadiliko makubwa katika sheria zake na
imeonyesha uwezo na utayari wa kusikiliza kesi zote zinazohamishiwa
nchini humo kutoka katika mahamakama hiyo. Munyagishari anashitakiwa kwa
makosa ya mauaji ya kimbari, kula njama kutenda mauaji hayo, kama kosa
mbadala, mauaji na ubakaji,kamamakosa ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Kesi ya Ngirabatware yaanza tena: Kesi inayomkabili aliyekuwa Waziri
wa Mipango nchiniRwanda, Augustin Ngirabatware ilianza tena kusilizwa
Jumanne wiki hii. Upande wa mashitaka uliita shahidi wake wa mwisho
ambaye ni mwanadiplomasia kutokaNigeria. Shadidi huyo ameletwa kupinga
utetezi wa mshitakiwa kuwa hakuwepo nchiniRwandakati ya Aprili 23 na Mei
23, 2012. Mahakama baadaye iliahirisha mahojiano ya utetezi kwa
shahidi huyo hadi Julai 2.
RWANDA
Mugesera atinga mahakamani bila wakili wake: Jumatatu wiki hii, Msomi
waKinyarwanda,LeonMugesera, alifika katika Mahakama Kuu mjiniKigalibila
kuongozana na wakili wake. Anapinga uamuzi wa kumkatalia kucheleweshwa
kesi yake. Kufuatia Mugesera kukosa uwakilishi wa kisheria, mahakama
iliahirisha shaurihilohadi Juni 11.
WIKI IJAYO
ICC
Jumatatu na Jumanne kutakuwepo na vikao vya kujadili
tarehe itakayofaa kuanza kusikilizwa kwa kesi zinazowakabili Wakenya
wanne wanaotuhumiwa kuhusika katika makosa yaliyotokana na vurugu baada
ya uchaguzi mkuu wa rais nchini Kenya Disemba 2007.
Siku moja baadaye (Jumatano) majaji wa mahakama hiyo
watasikiliza hoja za upande wa mashitaka na utetezi juu ya adhabu
anayostahili kupewa kiongozi wa waasi, Thomas Lubanga, ambaye ametiwa hatiani kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu.
RWANDA
Mshitakiwa wa mauaji ya kimbari, Leon Mugesera, anatarajiwa kufika tena mahakamani Jumatatu kujua mustakabali wa kesi yake.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia