Kama kawaida yao kwa machalii wa Arusha (A-Town) ni kwamba ukimzingua
chalii mmoja wa Arachuga tambua kuwa umemess up na mji mzima.
Kwa mujibu wa taarifa za uhakika toka A-TOWN ni kwamba kama Madee
asipoonyosha maelezo yake kuhusu haki ya Dogo Janja ama kuomba radhi kwa
walichomfanyia (Tip Top Connection), Arusha itakua chungu kwao. Kuna
wale wanaosema kuwa wakimwona Arusha basi atarudi Dar jina tu.
Wapenzi wa hip hop jijini Arusha wana hasira na Madee kwakuwa
wanaamini kuwa amemdhulumu Dogo Janja haki yake na kama asipoenda hewani
kukiri kosa lake mambo yanaweza kuwa magumu zaidi kwake.
Source: www.djnass255.blogspot.com