WATU WATANO WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 13 KUJERULIWA KATIKA AJALI MBILI TOFAUTI

Watu watano wamefariki dunia  na wengine  13 wamejeruhiwa vibaya kufuatia ajali   mbili tofauti zilizotokea  wilayani  hai  mkoani  kilimanjaro

Akizungumza mara baada ya kuwatembelea majeruhi wa ajali hiyo katika hospitali ya wilaya  ya Hai, mkuu wa wilaya ya hai Novatus Makunga amesema ajali ya kwanza  imetokea maeneo ya  mbosho wilayani humo  iliyohusisha   busi dogo aina ya Hiece  namba  T179 AAV baada ya kuacha njia na kupinduka
 
Bwana makunga ameeleza kuwa ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu watatu ambao amesema wamefariki papo hapo na wengine  13 kujeruhiwa vibaya

Mkuu huyo wa wilaya amewataja waliofariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni  Fred  Tarimo  miaka 23,  Elisinga  lema (90) na Raphael  kimaro  miaka haijulikani

Kuhusu ajali ya pili bwana  makunga amesema  imetokea eneo la  ango mjini boma ngombe   iliyohusisha  gari la maji aina ya isuzu lenye namba za usajili  T 125 BGY  kugongana na pikipiki maarufu kama bodaboda na kusababisha  kifo cha mwendesha pikipiki papo hapo


  Dreva  wa pikipikihiyo aliyetambuliwa na jina la rabi urassa miaka 35 amefariki papo hapo . amesema mkuu huyo wa wilaya

Aidha makunga  abiria  aliyekuwa   amechukuliwa na pikipiki hiyo pia amefariki hapo hapo  hadi sasa bado  hajatambuliwa

Mkuu huyo wa wilaya amefafanua kuwa  majeruhi watano kati ya 13  wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya hai

 Amesema  majeruhi  nane wamelazwa  katika hospitali ya rufaa  ya kcmc  kutokana na hali zao kuwa mbaya
Akizungmza kwa njia ya simu , mganga mkuu wa hospitali ya  mawenzi   dkt  Paul Chawote  amekiri kupokea maiti  za watu watano waliofariki katika ajali hizo mbili


Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa kilimanjaro  ramadhan nganzi  amekiri kutkea kwa ajali hizi mbili na kwamba jeshi la polisi linawasaka madreva wawili  akiwemo wa lori la  isuzu na  dreva wa hirce

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post