MSIMAMIZI wa
kundi la muziki la Contagious lenye makazi yake jijini Arusha,Njara
Rasolomanana maarufu kama Dady amevamiwa na kundi la majambazi nyumbani kwake
Kimandulo jijini hapa ambapo alijeruhiwa na kisha kuporwa vitu mbalimbali vyevye thamani ya kiasi cha zaidi ya sh,12 milioni.
Tukio hilo
lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya saa 1.30 asubuhi ambapo kundi la majambazi 17 wakitumia jiwe aina ya fatuma
walivunja mlango wake na kisha kumjeruhi kabla ya kumpora vitu mbalimbali.
Akihojiwa na libeneke la kaskazini huku akionyesha majeraha katika eneo la uso na mgongo
wake,Rasolomanana alisema kwamba wezi hao walifanikiwa kumpora simu
tano,kompyuta ndogo tatu,na kiasi cha sh,4 milioni.
Njara
,ambaye ni raia wa Madagascar alisema kwamba tayari ameshafungua jalada la tukio
hilo katika kituo kikuu cha polisi cha kati jijini Arusha na kupewa nambari za
AR|RB|7548|2012 .
Kamanda mkuu
wa jeshi la polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema kwamba jeshi lake bado linafuatilia kwa kina tukio hilo
kwa lengo la kuwashikilia watuhumiwa.