MJI MDOGO WA NGARAMOTONI WAONGOZA KWA UCHAFU ARUSHA
MJI mdogo wa
Ngaramtoni Wilayani Arusha Vijijini upo hatarini kukumbwa na Magonjwa ya
Mlipuko (Kipindupindu)hasa katika nyakati hizi za Mvua kali kutokana na baadhi
ya maeneo ndani ya mji huo kukumbwa na uchafu
Akiongea na Libeneke la kaskazini mkazi wa eneo hilo kwa niaba ya wananchi wa eneo hilo James
Mrutu alisema kuwa mji huo kwa sasa una uchafu mwingi sana hali ambayo
inahatarisha afya za wakazi wa eneo hilo
Alisema kuwa hapo awali kulikuwa na utaratibu mzuri sana wa kuzoa taka katika maeneo mbalimbali lakini kwa
sasa utaratibu huo haufuatwi na badala yake taka zimekuwa zikisagaa ovyo huku
zikitoa harufu mbaya sana
Aliongeza kuwa endapo
kama hali hiyo ya uzoaji wa taka kwa haraka haitaweza kufuatwa basi taka hizo
zinaweza kusababisha matatizo makubwa ya magonjwa ya mlipuko kama vile homa ya
matumbo(TYPHOID)na Kipindupindu jambo ambalo nalo litakuwa ni chanzo kikubwa
sana cha umaskini
Aliziomba mamlaka husika kuhakikisha kuwa zinazingatia zoezi
zima la uzoaji wa Taka ambapo hapo awali kulikuwa na utaratibu wa kutupa taka
kwa kutumia magari maalumu tofauti na sasa ambapo wananchi walio wengi
wanakusanya taka hizo kila siku huku gari nalo likiwa halina utaratibu wa
kupita mara kwa mara .
Awali diwani wa eneo hilo bw
David Kinisi alithibitisha kuwepo kwa changamoto hiyo ya kukithiri kwa ongezeko
kubwa sana la
uchafu katika mji mdogo wa Ngaramtoni na kusema kuwa wahusika wanaweka mji huo
pabaya
kinisi alifafanua kuwa endapo kama hali hiyo itaendelea
ni wazi kuwa Madhari ya mji huo itakuwa na mtizamo wa tofauti sana hali ambayo
nayo itachangia kukithiri kwa magonjwa,pamoja na umaskini mkubwa ambao unaletwa
na uchafu
Alizitaka mamlaka husika kuhakikisha kuwa zinafanya mara
moja zoezi hilo na kuweza kuokoa madhari ya Mji
huo wa Ngaramtoni kwa kuwa hapo awali Mji huo ulikuwa ni miongoni mwa Miji
yenye sifa za usafi sana
katika halmashauri hiyo ya Arusha
Vijijini.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia