EAC ANTHEM,UJUE WIMBO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI



Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kutoka kushito: Yoweri Museveni (Uganda), Mwai Kibaki (Kenya), Paul Kagame (Rwanda), Jakaya Kiwete (Tanzania) na Pierre Nkurunziza (Burundi)
 
Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.

1. Ee Mungu twakuomba ulinde
Jumuiya Afrika Mashariki
Tuwezeshe kuishi kwa amani
Tutimize na malengo yetu.

2. Uzalendo pia mshikamano
Viwe msingi wa Umoja wetu
Natulinde Uhuru na Amani
Mila zetu na desturi zetu.

3. Viwandani na hata mashambani
Tufanye kazi sote kwa makini
Tujitoe kwa hali na mali
Tuijenge Jumuiya bora.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post