KARIBU FAIR BONANZA YAMALIZIKA
Diwani aliyejiuzuru anafahamika kwa jina la Rasta akiwa ana badilishana mawazo na meya Gaudence lyimo
Meya akikagua timu
mwenyekiti wa tato ambaye ni mbunge wa jimbo la mbulu akunay akiwa anabadilishana mawazo na meya wa jimbo la arusha mjini Gaudence Lyimo
washabiki wa timu ya Zara tours wakishangilia mara baada yakunyakua kombe
| watu walijiburudisha balaa |
Akiongea na waandishi wa habari meya wa manispaa ya Arusha Gaudence Lyimo alisema kuwa kiwanja hicho ambacho kwa sasa hakina vigezo vya kutosha kinatarajiwa kuanza kukarabatiwa hivi karibuni .
Alibainisha kuwa kutokana na uwanja huo kutokuwa na hali ya kuridhisha hali inayosababisha hata timu nyingi kubwa kushindwa kuweka kambi jijini hapa kutokana na ubovu wa viwanja hivyo wao kama manispaa wameamua kuingilia kati na kufanyia marekebisho uwanja huo.
"kiukwelii uwanja ni mbovu haundani na jiji letu kwani uwanja unavichuguu vingi ,vyoo vyake havirizishi , pia ubovu huu umesabisha ata timu nyingi kukimbia kunakipindi timu za nje ya nchi zilikuwa zinataka kuja kuweka kambi hapa lakini inashindikana kwa ajili ya uwanja mbali na timu za nje pia kuna timu za hapa nyumbani kama simba na yanga wanatani kuja maana hali ya hewa ni nzuri lakini uwanja unatuangusha"alisema Lyimo
Aidha alibainisha kuwa mpaka sasa watu wameshachaguliwa kusimamia swala hilo na kampuni ya Arusha City Trading Cetre co ltd imepewa dhamana ya kufanya kazi hii ikiwa ipo chini ya timu ya watu wasita waliopewa dhamana ya kusimamia kazi hiyi.
Alitaja watu waliopo katika kamati hiyo kuwa ni pamoja na yeye mwenyekiti Gaudence lyimo,Juma Losini,Aronta Kanombe,Nyama gege,Charles Kalebu Mwigoro pamoja na John Danelson Palanjo wote hawa wakiwa wanasimamia kazi hiyo.
Alibainisha mbali na hivi pia wanampango wa kutengeneza viwanja vingine pia ambavyo vitawasaidia na kuwawezesha vijana kupata viwanja vingi vitakavyo wasaidia kuchezea na kujifunza michezo mbalimbali.
Lyimo alibainisha kuwa wanampango wa kuwa na viwanja zaidi wa vitano vya michezo kwa mwaka huu ambapo wanamatumaini watavijenga.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia