BENKI YA NMB KANDA YA KASKAZINI YAWAPA MAFUNZO WATEJA WAO
Meneja wa NMB kanda ya kaskazini,Vick Bishubu akifuatiwa na Mwenyekiti
wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB,Adam Shayo( kulia) j ,wakijumuika
kumsikiliza kwa makini mtoa (hayupo pichani)katika semina ya siku moja
kwa klabu ya wafanyabiashara wa NMB wa mkoa wa Arusha
Baadhi ya wanachama wa klabu ya wafanyabiashara wateja wa NMB
wakifuatilia kwa makini mafunzo ya utafutaji masokob yaliyokuwa
yakitolewa
Meneja wa NMB kanda ya kaskazini ,Vicky Bishibo wa pili kutoka kushoto
akifuatilia kwa makini mafunzo ya ujasiriamali yaliyokuwa yakitolewa kwa
klabu ya wafanyabaishara wa NMB ,katika hotel ya Golden Rose jijini
Arusha
BENKI ya NMB kanda ya kaskazini imeanza kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wateja wake waliopo
kwenye klabu ya wafanyanyabiashara wa NMB katika mikoa ya kanda ya kaskazini
yanayolenga kuwajengea uwezo namna ya kutafuta masoko ili kuboresha biashara
zao.
Meneja wa NMB kanda ya kaskazini , Vicky Bishubo
aliyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa klabu ya wafanyabiashara
wa NMB ,150 kutoka mkoa wa Arusha.
Alisema kuwa, mafunzo hayo yamekuwa yakiwasaidia kupata
mbinu za kibiashara na fedha na kupanua uwezo katika utafutaji wa masoko na
hivyo kuwawezesha kumudu urejeshaji wa
mikopo kwa wakati pindi wanapokopa .
Bishubo
alifafanua kuwa mafunzo hayo ,yamekuwa yakitolewa kila mwaka , yamesaidia
kuwaunganisha wafanyabiashara na benki katika kupata mikopo na kuirejesha kwa
wakati.
Aidha
alisema mafunzo hayo yatatolewa pia kwa vilabu vya wateja wa NMB
waliopo kwenye mikoa ya Kilimanjaro na Tanga wiki hii,ambapo vilabu vya
benki hiyo kanda ya kaskazini vinawanachama zaidia 450 ambao wamekuwa
wakinufaika na mafunzo hayo kila mwaka.
Naye
mwenyekiti wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB ,Adamu Shayo alisema kuwa
mafunzo hayo yamewasaidia sana kuwajengea uwezo wa kibiashara kupanua
wigo wa biashara zao ukizingatia nchi ya Tanzania sio kisiwa.
Alisema biashara zao zimekuwa zikiingiliana na wenzao kote ulimwenguni katika kutafuta
masoko ya ndani na nje,hivyo mafunzo kama hayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa
kuwajengea uwezo wa kutafuta masoko.
Alisema
kuwa mafunzo haya yamekuja wakati mwafaka kwa sababu mipaka ya Nchi za Afrika
mashariki inafunguliwa na utandawazi unaenea kwa kasi na itasaidia kufaidika na
soko la pamoja la jumuiya ya Afrika masharika.
Shayo
ambaye ni mmiliki wa chuo cha ualimu Sila(Sila Teachers College) chenye namba
ya usajili CU 115 kinachotoa cheti cha
grade A ya ualimu na ajira moja kwa moja ndani ya serikali ,alisema ameweza
kunufanika na mikopo ya benki ya NMB kupitia klabu ya wafanyabiashara na
kuweza kujenga chuo hicho chenye kiwango
cha kimataifa.
Mafunzo hayo yateendelea kwenye mikoa ya Kilimanjaro ,Manyara
na Tanga a,mbapo kwa kupitia vilabu vya wafanyabaishara,wateja wa NMB watapata
fursa ya kupata mafunzo hayo .
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia